عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لاَ يَنْظُرُ اللَّهُ إِلَى مَنْ جَرَّ ثَوْبَهُ خُيَلاَءَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5783]
المزيــد ...
Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema:
"Hamtazami Mwenyezi Mungu mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5783]
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuburuza nguo au kikoi chini ya kongo mbili kwa kiburi na kujiona, nakuwa mwenye kufanya hivyo atastahiki ahadi ya adhabu kali yakuwa Mwenyezi Mungu hatomtazama siku ya Kiyama mtazamo wa huruma.