عن حذيفة رضي الله عنه قال: سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول:
«لَا يَدْخُلُ الْجَنَّةَ قَتَّاتٌ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6056]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Haingii peponi mfitinishaji".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake] - [Swahiih Al Bukhaariy - 6056]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mmbea anayehamisha maneno kati ya watu kwa lengo la kuwavuruga kati yao yakuwa anastahiki adhabu kwa kutoingia peponi.

Katika Faida za Hadithi

  1. Umbea ni katika madhambi makubwa.
  2. Katazo la umbea; kwani ndani yake kuna kuwavuruga watu na madhara baina ya mtu na mtu na jamii mzima.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (67)