عن عُقبة بن عامر الجُهني رضي الله عنه قال: قال رسولُ الله صلَّى الله عليه وسلم:
«الجاهِرُ بالقرآن كالجاهِرِ بالصَّدَقَةِ، والمُسِرُّ بالقرآن كالمُسِرِّ بالصَّدَقَة».
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي] - [سنن أبي داود: 1333]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Uqbah Bin Aamir Al-juhaniy-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake:
"Mwenye kuisoma Qur'ani kwa sauti ya wazi ni kama mwenye kutoa sadaka hadharani, na mwenye kuisoma Qur'ani kwa siri ni kama mwenye kuficha sadaka."
[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 1333]
Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kuweka wazi kusoma Qur'ani ni sawa na mwenye kuweka wazi anapotoa sadaka, na mwenye kuficha kisomo cha Qur'ani ni sawa na mwenye kuificha sadaka.