عَنْ مَعْقِلِ بْنِ يَسَارٍ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«الْعِبَادَةُ فِي الْهَرْجِ كَهِجْرَةٍ إِلَيَّ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2948]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ma'qal bin Yasari -radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Kufanya ibada katika (nyakati) za vita vurugu na mauaji ni kama kuhama kuja kwangu".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2948]
Ameelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika nyakati za vurugu na fitina na mauaji na kuparaganyika kwa mambo ya watu katika ibada na kushikamana nayo, na kwamba malipo yake ni kama kuhama kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hii ni kwa sababu watu hughafilika nayo, na hawatengi muda ila mtu mmoja mmoja.