عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«أَيُحِبُّ أَحَدُكُمْ إِذَا رَجَعَ إِلَى أَهْلِهِ أَنْ يَجِدَ فِيهِ ثَلَاثَ خَلِفَاتٍ عِظَامٍ سِمَانٍ؟» قُلْنَا: نَعَمْ. قَالَ: «فَثَلَاثُ آيَاتٍ يَقْرَأُ بِهِنَّ أَحَدُكُمْ فِي صَلَاتِهِ خَيْرٌ لَهُ مِنْ ثَلَاثِ خَلِفَاتٍ عِظَامٍ سِمَانٍ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 802]
المزيــد ...
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Je anapenda mmoja wenu pindi atakaporudi kwa mke wake apate Ngamia watatu wenye mimba na walio nenepa?" Tukasema: Ndiy. Akasema: "Basi aya tatu anazozisoma mmoja wenu katika sala zake ni bora kwake kuliko Ngamia watatu wenye mimba na walionenepa."
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 802]
Anaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa malipo ya kusoma Aya tatu katika sala; ni bora kuliko mtu kupata nyumbani kwake Ngamia wakubwa wenye mimba na walio nenepa.