عَنِ ‌ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا قَالَ:
كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَليهِ وَسَلَّمَ لا يَعْرِفُ فَصْلَ السُّورةِ حَتَّى تَنْزِلَ عَليْهِ {بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ}.

[صحيح] - [رواه أبو داود] - [سنن أبي داود: 788]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema:
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hajui kitenganishi kati ya Sura na Sura nyingine mpaka imteremkie {Bismillahir Rahmanir Rahiim}.

[Sahihi] - [Imepokelewa na Abu Daud] - [Sunanu Abii Daud - 788]

Ufafanuzi

Anaweka wazi Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: kuwa Sura za Qur'ani tukufu zilikuwa zikiteremka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- haikuwa ikijulikana kitenganishi chake wala mwisho wake mpaka imteremkie: {Bismillahir Rahmanir Rahiim} basi wakati huo ndipo hujua kuwa Sura iliyotangulia imekwisha, na hiyo Bismillahi ni mwanzo wa Sura mpya.

Katika Faida za Hadithi

  1. Bismillah hutumika kuzitenganisha Sura, isipokuwa kati ya Suratul Anfaal na Suratu t-taubah.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (65)
Ziada