عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ قَالَ: سُبْحَانَ اللَّهِ وَبِحَمْدِهِ في يومٍ مِائَةَ مَرَّةٍ حُطَّتْ عَنْهُ خَطَايَاهُ وَإِنْ كَانَتْ مِثْلَ زَبَدِ الْبَحْرِ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, Amesema: "Atakayesema: Sub-haana llaahi wabihamdihi- Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake- kwa siku mara mia moja, atasamehewa makosa yake hata kama yatakuwa mfano wa povu la bahari".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Katika hadithi kuna dalili juu ya fadhila za dhikiri hii iliyokusanya kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa namna hii, nakuwa atakayeileta hiyo hakika Mwenyezi Mungu atamfutia madhambi yake vyovyote yatakavyokuwa mengi, hata kama yatafikia mfano wa povu la bahari katika wingi, ni fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake wenye kumtaja. Nayo ni katika nyiradi za asubuhi kwa kile kilicho elezwa katika hadithi: "Katika siku" na ni katika nyiradi za jioni pia, kwa hadithi ya Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake: "Atakayesema wakati ameamka na wakati ameshinda: Sub-haana llaahi wabihamdihi- Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake- mara mia moja, hatokuja yeyote siku kiyama na kitu bora kuliko alichokuja nacho, ispokuwa mtu aliyesema kama alivyosema au akazidisha" kaipokea Muslim.