عن أبي أيوب رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ قَالَ: لَا إلَهَ إلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ، وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ عَشْرَ مَرَّاتٍ كَانَ كَمَنْ أَعْتَقَ أَرْبَعَةَ أَنْفُسٍ مِنْ وَلَدِ إسْمَاعِيلَ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abii Ayubu- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Atakayesema: Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul Mulku walahul Hamdu, Wahuwa a'laa kulli shay in Qadiir (Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika, Ufalme ni wake, na sifa njema ni zake, Naye juu ya kila kitu ni muweza), akasema hivyo mara kumi, Atakuwa sawa na aliyeacha huru nafsi nne katika watoto wa Ismail".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Hadithi hii ni dalili juu ya ubora wa kumtaja Mwenyezi Mungu kwa yale yaliyomo miongoni mwa kukiri Tauhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu), nakuwa atakayesema mara kumi kwa kujua maana yake na kwa kufanyia kazi malengo yake atakuwa na malipo mfano wa malipo ya aliyeacha huru watumwa wanne kutoka katika kizazi cha Ismail bin Ibrahim -Ziwe juu yao sala na salamu.