عن معاوية بن أبي سفيان رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «من يُرِدِ الله به خيرا يُفَقِّهْهُ في الدين».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Muawiya bin Abii Sufiyani- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani zimfikie: "Mwenye kumtakia Mwenyezi Mungu kheri kwake humpa ufahamu katika dini".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Mwenye kumtakia Mwenyezi Mungu kwake manufaa na kheri anamfanya kuwa mtambuzi wa hukumu za kisheria mwenye maarifa ndani yake, Na Ufahamu una maana mbili: wa kwanza: kuzijua hukumu za kisheria za kielimu kutoka katika dalili zake zilizofafanuliwa, kama hukumu za ibada na miamala, Ya pili: Elimu ya dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu moja kwa moja, inayo kusanya misingi ya imani na sheria za uislamu na kujua halali na haramu na tabia na adabu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Katika hadithi kuna dalili juu ya utukufu wa kuwa na ufahamu katika dini na kuhimizwa juu yake.
  2. Nikuwa Ufahamu una maana mbili: Elimu ya hukumu za kisheria zilizofafanuliwa, na kutoka katika dalili zake zilizofafanuliwa, Na ya pili: Elimu ya dini ya Mwenyezi Mungu moja kwa moja ya misingi ya imani, na sheria za uislamu, na uhalisia wa ihsani (wema) na kujua halali na haramu.
  3. Tunafaidika kutoka katika hadithi pia kuwa atakayepuuza kuijua dini basi Mwenyezi Mungu Mtukufu hajamtakia kheri.
  4. Atakayeipupia elimu basi Mwenyezi Mungu anampenda, kwani Mwenyezi Mungu kamtakia kheri kwa kumuafikisha kwake katika elimu na utambuzi katika dini.
  5. Hakika ufahamu katika dini ni jambo la kusifiwa, ama ufahamu katika mengine yasiyokuwa dini hausifiwi wala hausemwi vibaya, ispokuwa utakapokuwa ni njia ya kitu chenye kusifiwa utasifiwa, na ukiwa ni njia ya kitu chenye kusemwa vibaya utasemwa vibaya.