عَنْ سَفِينَةَ رَضيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ:
كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُغَسِّلُهُ الصَّاعُ مِنَ المَاءِ مِنَ الجَنَابَةِ، وَيُوَضِّئُهُ المُدُّ.
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 326]
المزيــد ...
Kutoka kwa Safina radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kikimuosha kibaba cha maji kutokana na janaba, na ukimtia udhu ujazo wa kiganja.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 326]
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akioga kutokana na janaba kwa kiasi cha kibaba, na akitawadha kwa ujazo wa kiganja, na kibaba: Ni ujazo wa viganja vinne, na kiganja: Ni kiasi cha ujazo wa viganja viwili vya mtu wa maumbile ya kati na kati.