عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ رَفَعَهُ:
فِي قَوْلِ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ: {وَمَنْ يُرِدْ فِيهِ بِإِلْحَادٍ بِظُلْمٍ نُذِقْهُ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ} [الحج: 25] قَالَ: «لَوْ أَنَّ رَجُلًا هَمَّ فِيهِ بِإِلْحَادٍ وَهُوَ بِعَدَنِ أَبْيَنَ لَأَذَاقَهُ اللَّهُ عَذَابًا أَلِيمًا».
[صحيح] - [رواه أحمد والحاكم] - [المستدرك على الصحيحين: 3461]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake (Hadithi Marfu'u):
Katika kauli yake Aliyetakasika na kutukuka: "Na yeyote anayetaka, ndani ya Msikiti Mtukufu, kwenda kombo na haki kwa njia ya udhalimu na akamuasi Mwenyezi Mungu humo ndani, basi tutamuonjesha adhabu kali yenye kuumiza" [Al-Hajji:25] Akasema: "Lau kama mtu atadhamiria ubaya akiwa katika mji wa eden (Yemen) mbali huko, basi Mwenyezi Mungu angemuonjesha adhabu chungu".
[Sahihi] - - [المستدرك على الصحيحين - 3461]
Ameeleza Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake katika kauli yake Aliyetakasika na kutukuka: "Na yeyote anayetaka, ndani ya Msikiti Mtukufu, kwenda kombo na haki kwa njia ya udhalimu na akamuasi Mwenyezi Mungu humo ndani, basi tutamuonjesha adhabu kali yenye kuumiza" [Al-Hajji: 25], akasema: Lau mtu yeyote atawaza ndani ya nafsi yake na akaazimia kufanya jambo baya ndani ya sehemu tukufu ya Makka, likahalalishwa ndani yake aliloliharamisha Mwenyezi Mungu, kama makosa ya ulimi au kuuwa kwa makusudi, basi hiyo ni dhulma, hata kama maazimio atayaweka akiwa katika mji wa Eden huko Yemen, basi huyu atastahiki Mwenyezi Mungu amuonjeshe adhabu chungu kwa sababu ya hilo, hata kama hajalifanya, maazimio yake katika hilo yanatosha.