+ -

عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضيَ اللهُ عنهُما قَالَ:
كُنْتُ عِنْدَ مِنْبَرِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ رَجُلٌ: مَا أُبَالِي أَلَّا أَعْمَلَ عَمَلًا بَعْدَ الإِسْلَامِ إِلَّا أَنْ أُسْقِيَ الحَاجَّ، وَقَالَ آخَرُ: مَا أُبَالِي أَلَّا أَعْمَلَ عَمَلًا بَعْدَ الإِسْلَامِ إِلَّا أَنْ أَعْمُرَ المَسْجِدَ الحَرَامَ، وَقَالَ آخَرُ: الجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ أَفْضَلُ مِمَّا قُلْتُمْ، فَزَجَرَهُمْ عُمَرُ، وَقَالَ: لَا تَرْفَعُوا أَصْوَاتَكُمْ عِنْدَ مِنْبَرِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ يَوْمُ الجُمُعَةِ، وَلَكِنْ إِذَا صَلَّيْتُ الجُمُعَةَ دَخَلْتُ فَاسْتَفْتَيْتُهُ فِيمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ، فَأَنْزَلَ اللهُ عَزَّ وَجَلَّ: {أَجَعَلْتُمْ سِقَايَةَ الْحَاجِّ وَعِمَارَةَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ كَمَنْ آمَنَ بِاللهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ} [التوبة: 19] الآيَةَ إِلَى آخِرِهَا.

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1879]
المزيــد ...

Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao amesema:
Nilikuwa katika Mimbari ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mtu mmoja akasema, si jali ni amali gani nitakayoifanya baada ya Uislamu isipokuwa nitawapa maji mahujaji, na mwingine akasema: Sijali kutofanya amali yoyote baada ya Uislamu isipokuwa nitauimarisha Msikiti mtukufu, na mwingine akasema: Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko yote mliyosema, Omari akawakemea, na akasema: Msinyanyue sauti zenu mbele ya Mimbari ya Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, na hali yakuwa pia ni Ijumaa, lakini nitakaposwali Ijumaa nitaingia na nitamuuliza kuhusu haya mliyotofautiana kwayo, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Mnayafanya, enyi watu, yale mnayoyasimamia ya kuwanwyesha mahujaji na kuuimarisha msikiti Mtukufu ni kama Imani ya aliyemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho? [Tauba: 19] Mpaka mwisho wa Aya.

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1879]

Ufafanuzi

Ameeleza Nuuman bin Bashiri radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, yakwamba alikuwa amekaa katika Mimbari ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akamsikia mtu mmoja akisema: Sijali kutofanya amali yoyote baada ya kusilimu kwangu isipokuwa nitawanywesha maji mahujaji. Na mwingine akasema: Na mimi sijali kutofanya amali yoyote baada ya kusilimu kwangu isipokuwa nitauimarisha Msikiti mtukufu, na akasema mwingine: Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ndio bora zaidi kuliko hayo mliyoyasema. Omari bin Khattwabi akawakemea kwa kunyanyua sauti zao mbele ya Mimbari ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na tukio hilo lilikuwa asubuhi ya siku ya Ijumaaa, lakini nitakaposwali Ijumaa nitaingia na nitamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika haya mliyotofautiana kwayo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akateremsha:
"Mnayafanya yale mnayoyasimamia ya kuwanwyesha mahujaji na kuuamirisha msikiti mtukufu ni kama imani ya aliyemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho na akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Haziwi sawa hali za Waumini na hali za makafiri mbele ya Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaelekezi watu wanaozidhulumu nafsi zao kwa ukafiri kwenye mambo mema." [At-Tauba: 19].

Katika Faida za Hadithi

  1. Matendo huzidiana katika malipo na thawabu.
  2. Kuzidiana kwa matendo hulingana na namna yalivyokuja katika sheria, na wala si kulingana na jitihada za watu.
  3. Ubora wa Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu kwa sharti la kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho.
  4. Amesema Nawawi: Hapa kuna karaha ya kunyanyua sauti katika misikiti siku ya Ijumaa na siku nyinginezo, na kwamba mtu haruhusiwi kunyanyua sauti si kwa swala la kielimu wala linginelo panapokuwa na mkusanyiko wa watu kwa ajili ya swala, kwa kuwa kufanya hivyo huwashawishi wengine, na wenye kuswali na wenye kumtaja Mwenyezi Mungu.
Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kibangali Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kireno Thai Kiassam الهولندية الدرية المجرية الجورجية المقدونية
Kuonyesha Tarjama