+ -

عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَفَاتِحُ الغَيْبِ خَمْسٌ، {إِنَّ اللَّهَ عِنْدَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَيُنْزِلُ الغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الأَرْحَامِ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَاذَا تَكْسِبُ غَدًا وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ}».

[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 4627]
المزيــد ...

Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema:
"Funguo za mambo ya ghaibu ni tano, "Hakika kuijua Saa ya Kiyama kuko kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ndiye anayeiteremsha mvua. Na anavijua vilivyo ndani ya matumbo ya uzazi. Na haijui nafsi yoyote itachuma nini kesho. Wala nafsi yoyote haijui itafia nchi gani. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua, Mwenye habari".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 4627]

Ufafanuzi

Ghaibu iko kwa Mwenyezi Mungu hakuna aijuaye ila Yeye, na ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa funguo za mambo yaliyofichikana na hazina zake ni tano: Ya kwanza: Hakuna ajuaye ni lini kitasimama Kiyama isipokuwa Mwenyezi Mungu, ikiashiria kuijua Akhera, kwani siku ya Kiyama ndio mwanzo wake, na ikikanushwa elimu ya kilicho karibu basi inashindikana elimu iliyo baada yake. Ya pili: Hakuna ajuaye ni lini inakuja mvua isipokuwa Mwenyezi Mungu, hii ikiashiria mambo ya ulimwengu wa juu, na ameitaja mvua pekee pamoja nakuwa inaweza kuwa na sababu zilizozoeleka zinazoweza kujulisha unyeshaji wake lakini hua hazina uhakika wala yakini. Ya tatu: Yanayokuwa katika mifuko ya uzazi; kama mwanaume au mwanamke, mweusi au mweupe, amekamilika maumbile au amepungua, muovu au mwema na mfano wake, na ametaja uzazi pekee kwa sababu kwa kawaida watu wengi wanaujua, pamoja na hivyo akakanusha yeyote kujua uhalisia wake basi kisichokuwa mfuko kutojulikana ndio bora zaidi. Ya nne: Hakuna ajuaye yaliyoko kesho isipokuwa Mwenyezi Mungu, ikiashiria aina za nyakati na matukio yaliyomo, na ameeleza kwa tamko "kesho" ili uhalisia wake uwe ni wakati wa karibu zaidi, na ikiwa pamoja na ukaribu wake hakuna ajuaye uhalisia wa yatakayotokea ndani yake, pamoja na kuwezekana kupata dalili na alama zake, basi siku baada yake ndio bora zaidi kutojulikana. La tano: Haijui nafsi itafia nchi gani, ikiashiria mambo ya ulimwengu wa chini, pamoja nakuwa kawaida watu wengi hufia katika nchi zao, lakini hilo si uhalisia, bali lau atakufa katika nchi yake pia hajui ni Ardhi gani atazikwa, hata kukiwa na makaburi ya watangulizi wake, "Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye habari" ameyazingira yenye kuonekana na yasiyoonekana, na yaliyofichikana na yaliyohifadhiwa, na siri zote, aya ikakusanya aina mbali mbali za ghaibu, na ikaondoa madai yote mabovu.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa kuwa hazina za ghaibu ni tano ambazo hakuna azijuaye isipokuwa Mwenyezi Mungu.
  2. Amesema Assindi: Kauli yake: "Funguo za mambo ya ghaibu ni tano", Yameitwa mambo haya matano: Funguo za ghaibu; kwa sababu mwenye kuwa na mambo haya matano basi anamiliki ghaibu yote, yakawa ni sawa na mambo yanayofunguliwa kwayo hazina za ghaibu.
  3. Amesema bin Hajari Abuu Hamza: Ameeleza kwa neno funguo ili kusogeza karibu jambo hili kwa msikilizaji; kwa sababu kila kitu kilichowekwa pazia baina yake na wewe basi kitakuwa kimefichika kwako, na kuweza kufikia kukijua kwa kawaida ni kupitia mlangoni, mlango ukifungwa itahitajika funguo, ikiwa kitu ambacho mtu hawezi kuona ghaibu isipokuwa kupitia hicho hajui mahali kilipo, ataweza vipi kujua ghaibu.
  4. Amesema bin Abii Hamza: Sababu na hekima ya kuyafanya kuwa ni mambo matano ni ishara ya kuwakusanya walimwengu ndani ya hayo.
  5. Inawezekana Mwenyezi Mungu kuwaonyesha ghaibu baadhi ya Mitume, kwa hekima toka kwake Mtukufu
  6. Ubatili ya tabiri za waaguzi na makuhani katika kujipa kwao kujua elimu ya ghaibu, na kwamba mwenye kudai kujua elimu ya mambo aliyojipwekesha nayo Mwenyezi Mungu kwa kuyajua, basi atakuwa amefanya muongo Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, na Qur'ani tukufu.
Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kibangali Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kireno Thai Kiassam الهولندية الدرية المجرية الجورجية المقدونية
Kuonyesha Tarjama
Ziada