عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَالِكٍ ابْنِ بُحَيْنَةَ رضي الله عنه:
أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا صَلَّى فَرَّجَ بَيْنَ يَدَيْهِ حَتَّى يَبْدُوَ بَيَاضُ إِبْطَيْهِ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 390]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdallah bin Maliki bin Buhaina radhi za Allah ziwe juu yake:
Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapo swali anatanua kati ya mikono yake mpaka unaonekana weupe wa kwapa zake.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 390]
Alikuwa rehema na amani zimshukie anaposwali, anaikunjua mikono yake wakati wa kusujudu. Alisogeza kila mkono kutoka upande wa karibu yake, kama mbawa mbili, mpaka rangi ya ngozi ya makwapa yake inaonekana; Hii ni katika kupitiliza kuitanua mikono na kuitenganisha na mbavu zake.