عَنْ عَمْرِو بْنِ الحَارِثِ خَتَنِ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَخِي أُمِّ المؤمِنين جُوَيْرِيَةَ بِنْتِ الحَارِثِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُم، قَالَ:
مَا تَرَكَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عِنْدَ مَوْتِهِ دِرْهَمًا وَلاَ دِينَارًا وَلاَ عَبْدًا وَلاَ أَمَةً وَلاَ شَيْئًا، إِلَّا بَغْلَتَهُ البَيْضَاءَ، وَسِلاَحَهُ، وَأَرْضًا جَعَلَهَا صَدَقَةً.
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 2739]
المزيــد ...
Kutoka kwa Amri bin Harithi shemeji yake na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kaka yake na mama wa waumini Juwairia binti Harithi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, amesema:
Hakuacha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati wa kifo chake Dirham moja wala Dinari, wala mtumwa wala kijakazi wala chochote, isipokuwa nyumbu wake mweupe, na silaha yake, na kipande cha Ardhi alichokitoa kama sadaka.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 2739]
Alifariki Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wala hakuacha Dirham ya fedha wala Dinari ya dhahabu, wala mtumwa mmilikiwa wala kijakazi mmilikiwa, wala mbuzi wala ngamia wala chochote katika mali, isipokuwa nyumbu wake mweupe aliyekuwa akimpanda, na silaha yake aliyokuwa akiibeba, na kipande cha Ardhi alichokitoa wakfu kwa ajili ya wasafiri.