Aina ndogo

Orodha ya Hadithi

1. Ya kwamba mwanamke mmoja alipatikana akiwa kauwawa katika moja ya vita vya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akakemea vikali Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuuwawa wanawake na watoto
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
2. Amekataza kuweka nadhiri, na akasema: "Hakika nadhiri haiji kwa kheri, bali hutolewa kwayo (vilivyo) kwa bahili
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
3. Wallahi – akipenda Mwenyezi Mungu - sitokula kiapo cha jambo fulani isipokuwa ninapoona kilichobora zaidi basi huwa ninatoa kafara ya kiapo changu kisha ninafanya lililo bora zaidi.” - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
4. Atakayevaa hariri duniani hatoivaa Akhera
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
5. Hakika katika Jihadi kubwa ni kusema neno la uadilifu kwa kiongozi dhalimu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
6. Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoamka usiku anasafisha kinywa chake kwa mswaki
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
7. Amekataza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuswali baada ya swala ya sub-hi mpaka lichomoze jua, na baada ya laasiri mpaka lizame
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
8. Yakuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Kiyama, akasema: Lini Kiyama? Akasema: “Umetayarisha nini kwa ajili yake?”
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
9. Mtu huwa katika mwenendo wa rafiki yake wa karibu, basi na aangalie mmoja wenu ni nani anayemfanya kuwa rafiki yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
10. Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.”
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
11. Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
12. “Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ole wao waarabu na watahadhari dhidi ya shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya'juuju na Ma'ajuju upenyo wa kiasi hiki.”
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
13. Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zaidi kuliko hata bikira ndani ya chumba chake, basi anapoona jambo asilolipenda tunajua kuwa hapendi kwa kupitia usoni kwake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
14. Atakayemuomba Mwenyezi Mungu shahada (yaani kufa shahidi) kwa dhati, basi atamfikisha daraja ya mashahidi hata kama atafia juu ya godoro lake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
15. Majaribio hayaachi kumpata muumini wa kiume na muumini wa kike katika nafsi yake, na watoto wake, na mali yake mpaka atakapokutana na Mwenyezi Mungu ilhali hana dhambi hata moja
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
16. Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja ni katikati ya usiku wa mwisho
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
17. Ataletwa mtu siku ya Kiyama, kisha atupwe motoni, ujiviringishe utumbo na vyote vilivyomo tumboni mwake, atazunguka nao (motoni) kama punda anavyozunguka na jiwe la kusagia nafaka
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
18. Hili ni jiwe lililotupwa Motoni muda wa (miaka) sabini iliyopita, na sasa linaanguka Motoni mpaka litafika katika kina chake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
19. Atakaye muandaa mpiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu basi na yeye atakuwa kapigana, na atakayemsimamia mpiganaji kwa wema katika familia yake basi na yeye atakuwa kapigana
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
20. Hakika mja anaweza kuzungumza neno asilijali ndani yake akateleza kwa neno hilo nakuingia katika moto ambao umbali wake ni baina ya mashariki na magharibi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
21. Hakuna Nabii aliyetumwa na Mwenyezi Mungu katika umma wowote kabla yangu, isipokuwa kunakuwa katika umma wake na watu wake wapendwa na watu wanaoyachukua mafundisho yake na wanafuata amri yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
22. Nimepewa mambo matano ambavyo hakupewa mtu mwingine miongoni mwa Manabii kabla yangu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
23. usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainni alaa dhikrika washukrika wahusni ibaadatika" Ewe Mwenyezi Mungu nisadie katika kukutaja na kukushukuru na kuzifanya vizuri ibada zako
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
24. Amesema Mwenyezi Mungu: Kila amali ya mwanadamu hiyo ni ya kwake isipokuwa swaumu, bila shaka hiyo ni yangu na mimi ndiye ninayeilipa - 10 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
25. Atakapokutana mmoja wenu na ndugu yake basi na amsalimie, ukiwatenganisha kati yao mti, au ukuta, au jiwe, kisha akakutana naye tena basi amsalimie tena
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
26. Anafunga shetani juu ya kisogo cha kichwa cha mmoja wenu, pindi anapolala, mafundo matatu, anafunga katika kila fundo usiku kucha na husema : basi lala
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
27. Macho ya aina mbili hautoyagusa moto: Jicho lililolia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, na jicho lililokesha likilinda kwaajili ya Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
28. Nilikutana na Ibrahimu usiku niliochukuliwa, Akasema: Ewe Muhammadi wafikishie umma wako salamu zangu, na uwaeleze kuwa pepo ina udongo mzuri, ina maji matam
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
29. "Umeniuliza kuhusu jambo kubwa, lakini nijepesi kwa yule atakayefanyiwa wepesi na Mwenyezi Mungu Mtukufu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
30. Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
31. Aliniusia mimi kipenzi changu -rehema na amani ziwe juu yake kwa mambo matatu: kufunga siku tatu katika kila mwezi, na rakaa mbili baada ya kuchomoza jua (Dhuhaa), na nisali witiri kabla sijalala
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
32. Mtakapouona basi fungeni, na mtakapouona basi fungueni, ukifunikwa kwenu nyinyi basi ukadirieni
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
33. Hakika katika yale waliyoyakuta watu miongoni mwa maneno ya kiutume ya mwanzo, usipokuwa na haya basi fanya ulitakalo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
34. Acha linalokutia shaka fanya lisilokutia shaka, kwani ukweli ni utulivu, na bila shaka uongo ni shaka
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
35. Kuwa duniani kama msafiri au mpitanjia
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
36. Ulimi wako usiache kuwa mbichi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
37. Usimuue, kwani ukimuuua basi yeye atakuwa katika nafasi yako kabla hujamuua, na wewe utakuwa katika nafasi yake kabla hajasema neno lake alilolisema
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
38. Atakayekula kitunguusaumu, au kitunguu maji, basi na ajitenge nasi, au ajitenge na msikiti wetu, na akae nyumbani kwake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
39. Hakika nitampa bendera hii mtu anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Mwenyezi Mungu ataleta ufunguzi kupitia mikono yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
40. Wasikilizeni na muwatii, kwani wao wana yao waliyobebeshwa nanyi mna yenu mliyobebeshwa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
41. Kumtukana Muislamu ni ufasiki (kutoka nje ya mipaka), na kupigana naye ni ukafiri
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
42. Msiwaanze Mayahudi wala wakristo kwa salam, mkikutana na mmoja wao njiani basi mbaneni mpaka adhikike
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
43. Si miongoni mwetu atakayepiga mashavu, na akachana mifuko, na akaomboleza kwa maombolezo ya watu wa zama za ujinga
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
44. Atakayekuja miongoni mwenu kwa ajili ya Ijumaa basi na aoge
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
45. Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakuniswalia - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
46. Atakayekwenda asubuhi msikitini au mchana, Mwenyezi Mungu humuandalia nyumba peponi kila anapotoka asubuhi au jioni
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
47. Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
48. Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
49. Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote, na yale unayoyajua kutoka kwangu, ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu, na yale ya makusudi na ujinga wangu na mzaha wangu, na hayo yote yaliyo kwangu, ewe Mola wangu nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza, wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji, na wewe juu ya kila kitu ni muweza
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
50. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
51. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutoka katika heri zote: zile za haraka na za kuchelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua, na ninajikinga kwako kutokana na shari zote zinazokuja haraka na zinazochelewa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
52. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kuondokewa neema zako, na kubadilika kwa afya yako, na kufikiwa ghafla na adhabu zako, na kila aina ya hasira zako
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
53. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutukanwa na maadui
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
54. Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka, na kwako tunashinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutakufa, na kwako tutafufuliwa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
55. Tahadharini sana na kuingia/kukaa kwa wanawake" Mtu mmoja katika Maanswari akasema: Ewe Mtume wa Allah vipi kuhusu shemeji? Akasema: "Shemeji ni kifo - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
56. Fedha kwa dhahabu ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na ngano isiyokobolewa ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na shairi (ngano iliyokobolewa ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na tende kwa tende ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
57. Sema: Ewe Mwenyezi Mungu niongoze na unisimamie, na kumbuka kwa uongofu ni kuongoka kwako njia, na kusimamiwa ni kusimamiwa kupatia (katika kila jambo lako mithili ya) mshale
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
58. Weka mkono wako juu ya mahala panapoumia katika mwili wako, na usema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mara tatu, na useme mara saba: Audhubillaahi wa quduratihi min sharri maa ajidu wa uhaadhiru (Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu na uwezo wake kutokana na shari ya kile ninachokipata na kile ninachokihofia)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
59. Yeyote atakayesema: Bismillaahi lladhi laa yadhurru ma'asmihi shai un fil Ardhwi walaa fis samaai, wahuwas samiiu'l 'aliim, (Kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye hakuna kinachoweza kudhuru pamoja na jina lake kitu chochote ardhini wala mbinguni, naye ni msikivu na mjuzi) mara tatu, basi halitomfika balaa la ghafla, mpaka atakapoamka
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
60. Kamwe, hatoingia motoni mtu yeyote aliyeswali kabla ya kuchomoza Jua na kabla ya kuzama kwake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
61. Hakuna yeyote atakayenisalimia isipokuwa Mwenyezi Mungu hunirudishia roho yangu ili nimjibu salam
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
62. Mambo mawili kwa watu hayo kwao ni ukafiri: Kutiana doa katika nasaba (ukoo), na kulia kwa kumuomboleza maiti
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
63. Hakuna mwenye kumiliki dhahabu wala fedha, na akawa hazitolei zaka zake, isipokuwa, pindi itakapofika siku ya Kiyama, atakunjiwa Sahani la kutoka motoni - 4 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
64. Atanadi mwenye kunadi: "Hakika, mtapata afya nzuri na wala hamtougua milele. Na hakika, mtakuwa hai na wala hamtokufa milele, na hakika mtakuwa vijana na wala hamtazeeka milele. Na hakika, mtastareheka na wala hamtapata shida yoyote milele
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
65. Wakati wakazi wa Peponi watakapoingia Peponi, Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, atasema: "Je, mnataka kitu chochote niwazidishie?
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
66. Ni safi Maji yake na ni halali mizoga yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
67. Maji yatakapokuwa ni kulataini (Mapipa mawili) basi hayashiki uchafu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
68. Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini mwake basi na apenge kwa maji mara tatu, kwani Shetani hulala ndani ya tundu zake za pua
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
69. Atakapotawadha mmoja wenu na akavaa khofu zake (au soksi zake) basi na aswali nazo, na afute juu yake kisha asizivue akitaka kufanya hivyo isipokuwa atakapokuwa na janaba
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
70. Hatomtuhumu mtu mwenzake kwa machafu, na wala hatomtuhumu kwa ukafiri, isipokuwa hurejea kwake, ikiwa ndugu yake hatokuwa hivyo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
71. Hakika shetani alishakata tamaa kuabudiwa na wenye kuswali katika kisiwa cha Arab, Lakini yuko katika kuwachochea baina yao
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
72. Atakayeiapia amana basi huyo si miongoni mwetu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
73. Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mimi nilionyeshwa kuwa nyinyi ndio wengi katika watu wa motoni" Wanawake wakasema: Na ni kwa nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Mnazidisha sana kulaani (kutukana) na mnawapinga waume, na mimi sijapata kuona wapungufu wa akili na dini wenye kuweza kuteka moyo ya mwanaume makini kuliko nyinyi - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
74. Atakayesema wakati anasikia adhana: Allaahumma rabba haadhihid da'watit taamma, was swalaatul qaaima, aati Muhammadanil wasiilata wal fadhwiila, wab'ath-huu maqaaman mahmuudanil ladhii wa a'ttah, (Ewe Mwenyezi Mungu, Mola wa wito huu uliotimia, na swala iliyosimama, mpe Muhammad utetezi na fadhila, na umfufue mahali pakusifiwa ulipomuahidi) basi utakuwa halali kwake utetezi wangu siku ya Kiyama
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
75. Asiswali mmoja wenu katika nguo moja ambayo hakuna chochote mabegani mwake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
76. Utakaposujudu basi weka viganja vyako, na unyanyue viwiko vyako
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
77. Niliswali pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa akitoa salaam kuliani kwake: "Assalaam alaikum warahamatullah wabarakaatuh", na kushotoni kwake: "Assalaam alaikum warahmatullah
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
78. Alisema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia Abubakari na Omari: "Hawa wawili ni mabosi wa watu wazima wa peponi kwanzia watu wa mwanzo na wa mwisho, isipokuwa Manabii na Mitume
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
79. Hassan na Hussein ni mabosi wa vijana wa peponi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
80. Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake alikuwa haziachi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa mbili kabla ya Alfajiri
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
81. Atakayehifadhi rakaa nne kabla ya Adhuhuri na rakaa nne baada yake basi Mwenyezi Mungu atamharamisha kuingia motoni
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
82. Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisoma katika rakaa mbili za (sunna ya) Alfajiri {Qul yaa ayyuhal kaafiruun} na {Qul huwallaahu ahad}
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
83. Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja akiswali peke yake nyuma ya safu, akamuamrisha arudie swala yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
84. Mwanamke yeyote atakayeolewa bila idhini ya walii wake, basi ndoa yake ni batili" Akasema hivyo mara tatu "Ikiwa atamuingilia basi mahari yake ndio itakuwa kwa ajili ya kile alichokifanya kwake, na ikiwa watazozona basi kiongozi ndiye msimamizi wa asiyekuwa na msimamizi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
85. Amelaaniwa mwenye kumuingilia mke wake kinyume na maumbile
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
86. Hamtazami Mwenyezi Mungu mtu ambaye kamuingilia mwanaume au mwanamke katika tupu yake ya nyuma
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
87. Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni zipi haki za mke wa mmoja wetu juu yake?, Akasema: "Ni umlishe pale unapokula, na umvishe unapovaa, au utakapopata kipato, na wala usipige uso, na wala usitoe maneno machafu, na wala usihame isipokuwa ndani ya nyumba
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
88. Atakayekuwa na wake wawili akaegemea kwa mmoja wao atakuja siku ya Kiyama upande wake mmoja ukiwa umepinda
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
89. Wapigeni vita washirikina kwa mali zenu na nafsi zenu na ndimi zenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
90. Kikoi cha muislamu kifikie nusu ya muundi, na wala hakuna tabu wala hakuna ubaya kikiwa kati yake na kati ya fundo mbili za miguu, kitakachokuwa chini ya fundo mbili basi hicho ni motoni, na atakayeburuza kikoi chake kwa kiburi hatomtazama Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu