Aina:
عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ بُسْرٍ رضي الله عنه أَنَّ رَجُلاً قَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ إِنَّ شَرَائِعَ الإِسْلاَمِ قَدْ كَثُرَتْ عَلَيَّ، فَأَخْبِرْنِي بِشَيْءٍ أَتَشَبَّثُ بِهِ، قَالَ:

«لاَ يَزَالُ لِسَانُكَ رَطْبًا مِنْ ذِكْرِ اللَّهِ».
[صحيح] - [رواه الترمذي وابن ماجه وأحمد] - [سنن الترمذي: 3375]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdallah bin Busri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba mtu mmoja alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika sheria za Uislamu zimekuwa nyingi kwangu, hebu nieleze kitu ambacho nitashikamana nacho, akasema:
"Ulimi wako usiache kuwa mbichi kwa kumtaja Mwenyezi Mungu".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad] - [Sunanu Tirmidhiy - 3375]

Ufafanuzi

Mtu mmoja alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ibada za sunna zimekuwa nyingi kwake mpaka zikamshinda kwa sababu ya udhaifu wake, kisha akamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake amuelekeze katika amali nyepesi itakayompa thawabu nyingi atakayoshikamana nayo na adumu nayo.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuelekeza kuwa ulimi wake uwe mbichi utikisike kwa kudumu kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu kila wakati na kila hali; kama kumsabihi na kumhimidi na kumtaka msamaha na kumuomba na mfano wake.

الملاحظة
مصدر
النص المقترح لا يوجد...
الملاحظة
مصدر
النص المقترح شَكَى رجلٌ إلى النبيِّ صلى الله عليه وسلم بأن نوافل العبادات قد كَثرت عليه حتى عجز عنها لضعفه، ثم سألَ النبيَّ صلى الله عليه وسلم أنْ يَدلَّه على عملٍ يسيرٍ مُسْتجلِبٍ لثواب كثير يتعلق به ويستمسك. فأرشده صلى الله عليه وسلم بأن يكون لسانه طَرِيًّا متحركًا من دوام ذكر الله سبحانه وتعالى في كل وقت وحال؛ من تسبيح وتحميد واستغفار ودعاء ونحو ذلك. https://hadeethenc.com/ar/browse/hadith/4716?note=1
الملاحظة
المصظر
النص المقترح شَكَى رجلٌ إلى النبيِّ صلى الله عليه وسلم بأن نوافل العبادات قد كَثرت عليه حتى عجز عنها لضعفه، ثم سألَ النبيَّ صلى الله عليه وسلم أنْ يَدلَّه على عملٍ يسيرٍ مُسْتجلِبٍ لثواب كثير يتعلق به ويستمسك. فأرشده صلى الله عليه وسلم بأن يكون لسانه طَرِيًّا متحركًا من دوام ذكر الله سبحانه وتعالى في كل وقت وحال؛ من تسبيح وتحميد واستغفار ودعاء ونحو ذلك. https://hadeethenc.com/ar/browse/hadith/4716

Katika Faida za Hadithi

  1. Fadhila za kudumu na kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  2. Miongoni mwa fadhila za Mwenyezi Mungu ni kufanya sababu za kupata malipo kuwa nyepesi.
  3. Watu kuzidiana katika mafungu yao katika milango ya wema na kheri.
  4. Kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi kwa ulimi, kwa kumsabihi na kumhimidi, na kukiri kuwa hapana mola muabudiwa wa haki ila yeye, na kumtukuza, na mengineyo pamoja na moyo kwenda sambamba na ulimi, hili linakaa nafasi ya ibada nyingi za sunna.
  5. Kuchunga kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake hali ya muulizaji kwa kumjibu kila linalomfaa.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (55)
Aina tofauti
Ziada