«إِنَّ مِنْ أَعْظَمِ الجِهَادِ كَلِمَةَ عَدْلٍ عِنْدَ سُلْطَانٍ جَائِرٍ».
[حسن لغيره] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه وأحمد]
المزيــد ...
kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudriy- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na Amani zimfikie, amesema: "Jihadi bora ni neno la uadilifu kwa kiongozi muovu".
Sahihi - Imepokelewa na Ibnu Maajah
Anabainisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba jihadi kubwa ya mtu ni kusema neno la haki kwa mwenye mamlaka dhalimu; kwasababu yeye huenda akamuadhibu kwasababu ya hilo na akamuudhi au akamuuwa, jihadi huwa kwa mkono kama kupigana na makafiri, na kwa ulimi kama kukemea dhulma, na kwa moyo kama jihadi ya nafsi.