أَنَّ امْرَأَةً وُجِدَتْ فِي بَعْضِ مَغَازِي النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَقْتُولَةً، فَأَنْكَرَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَتْلَ النِّسَاءِ وَالصِّبْيَانِ.
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdillah bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- "Yakwamba mwanamke mmoja alipatikana katika baadhi ya vita vya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiwa kauwawa, akakemea Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuuwa wanawake, na watoto wadogo".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Kukemea Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuuwa wanawake na watoto inaonyesha uharamu wa kuwauwa, na kauli yake katika baadhi ya hadithi zilizokuja katika maana hii: (Hakuwa huyu ni mwenye kupigana) ni angalizo juu ya sababu ya kukataza kuwauwa wanawake; kwasababu mara nyingi wao sio wenyekupigana, hata kama katika baadhi yao kuna shari na ushujaa, lakini hukumu imewekwa kwa wengi, atakayepigana atapigwa.