عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: إِنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ:

«إِذَا شَرِبَ الْكَلْبُ فِي إِنَاءِ أَحَدِكُمْ فَلْيَغْسِلْهُ سَبْعًا». ولمسلم: « أولاهُنَّ بالتُراب».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba" Na kwa Imamu Muslim: "Moja kati ya hizo kwa udongo". Na kutoka kwa Abdillah bin Maghfali -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "Atakapokunywa mbwa katika chombo basi kiosheni mara saba, na mkisugue mara ya nane kwa udongo".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

kwakuwa mbwa ni katika wanyama wanaokarahisha ambao wanabeba uchafu mwingi na maradhi, imeamrisha sheria tukufu kukiosha chombo ambacho amekunywa ndani yake mara saba, moja kati ya hizo iambatane na udongo ili maji yafuate baada yake, ili upatikane usafi kamili kutokana na najisi yake na madhara yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama

Maana ya Maneno