«كُنْ فِي الدُّنْيَا كَأَنَّكَ غَرِيبٌ أَوْ عَابِرُ سَبِيلٍ»، وَكَانَ ابْنُ عُمَرَ، يَقُولُ: إِذَا أَمْسَيْتَ فَلاَ تَنْتَظِرِ الصَّبَاحَ، وَإِذَا أَصْبَحْتَ فَلاَ تَنْتَظِرِ المَسَاءَ، وَخُذْ مِنْ صِحَّتِكَ لِمَرَضِكَ، وَمِنْ حَيَاتِكَ لِمَوْتِكَ.
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 6416]
المزيــد ...
kutoka kwa Abdullahi bin Amry -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alishika Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- bega langu, na akasema:
"Kuwa duniani kama msafiri au mpitanjia", Na alikuwa bin Omari akisema: Ukishinda mchana usisubiri asubuhi, na ukiamka asubuhi usisubiri jioni, na chukua fursa ya kuitumia vizuri afya yako kwa ajili ya maradhi yako, na uhai wako kwa ajili ya kifo chako.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 6416]
Ibn Omari Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, ameeleza kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimshika begani - nacho ni kiungo cha juu cha mkono na bega - akamwambia: Kuwa katika dunia hii kana kwamba wewe ni mgeni aliyekuja katika nchi ambapo hakuwa na makazi yake, na hakuna wakazi wa kumkaribisha wala familia tegemezi, wala mahusiano ambayo ni sababu ya hili, kuwa shupavu zaidi kuliko mgeni huyu ambaye ni mpita njia anayepita njiani kuelekea katika nchi yake. Kwa sababu mgeni anaweza kuishi katika nchi ya kigeni na akawa mkazi ndani yake, tofauti na msafiri anayetaka kwenda nchini kwake, haja yake huwa ni kupumzika ili apate wepesi na sio kukaa, na kuwa na hamu ya kuwasili katika nchi yake kama vile msafiri hahitaji zaidi ya yale yatakayomfikisha mwisho wa safari yake, halikadhalika muumini katika ulimwengu huu hahitaji zaidi ya yale yatakayomfikisha mahali pazuri.
Akazifanyia kazi bin Omari nasaha hizi na alikuwa akisema: Ukiamka usisubiri jioni, na ukishinda mpaka jioni usisubiri asubuhi, na ihesabu nafsi yako kuwa katika wafu walioko makaburini, na kwakuwa umri haukosi moja katika ya mawili, afya na maradhi; fanya haraka siku za afya yako kwa kufanya ibada kwa ajili ya maradhi yako; na tumia fursa ya matendo mema katika wakati wa afya kabla maradhi hayajakuzuia, na faidika na uhai wako katika dunia, kusanya ndani yake yale yatakayokunufaisha baada ya kifo chako.