كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُكْثِرُ أَنْ يَقُولَ: «يَا مُقَلِّبَ القُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِكَ»، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ، آمَنَّا بِكَ وَبِمَا جِئْتَ بِهِ فَهَلْ تَخَافُ عَلَيْنَا؟ قَالَ: «نَعَمْ، إِنَّ القُلُوبَ بَيْنَ أُصْبُعَيْنِ مِنْ أَصَابِعِ اللهِ يُقَلِّبُهَا كَيْفَ يَشَاءُ».
[صحيح] - [رواه الترمذي وأحمد]
المزيــد ...
Kutoka kwa Shahri bin Haushab Amesema: Nilisema kumwambia ummu salama -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-, Ewe mama wa waumini, Ni dua ipi alikuwa akiisoma zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapokuwa kwako? Akasema: Ilikuwa dua yake zaidi ni: "Ewe mwenye kuzigeuza nyoyo uthibitishe moyo wangu katika Dini yako".
Ni sahihi kwa sababu ya hadithi nyingine - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy
Ilikuwa dua yake zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake nikusema kauli hii: (Ewe mwenye kuzigeuza nyoyo) Yaani mwenye kuziendesha wakati mwingine katika utiifu na wakati mwingine katika maasi na kughafilika, (uthibitishe moyo wangu katika Dini yako) Yaani ufanye uthibiti katika dini yako usipinde katika dini madhubuti na njia iliyonyooka.