Aina ndogo

Orodha ya Hadithi

1. Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni msije kuapa (kupitia) kwa baba zenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
2. La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
3. Alipita Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili, Akasema: Hakika hawa wawili wanaadhibiwa, na hawadhibiwi kwa madhambi makubwa; ama mmoja wao: alikuwa hajisitiri kutokana na mkojo, na ama huyu mwingine: Alikuwa akitembea akiwafitinisha watu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
4. Mtakapomsikia muadhini basi semeni mfano wa jinsi anavyosema
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
5. Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika safari, nikanyoosha mikono ili nimvue viatu vyake (khufu), akasema; ziache; kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi, akafuta juu yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
6. Yakwamba Fatuma bint Abii Hubaishi: Alimuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akasema: Hakika mimi napata hedhi na wala sitwahariki, je niache swala? Akasema: Hapana usiache sala, Hakika huo niupasukaji wa mshipa, lakini acha swala kiasi cha siku ambazo ulikuwa ukiingia katika hedhi, kisha oga na uswali
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
7. Atakapotawadha mmoja wenu basi na aweke puani mwake maji, kisha apenge, na atakayestanji kwa mawe basi ayafanye kuwa witiri, na atakapoamka mmoja wenu toka usingizini mwake basi na aoshe mikono yake kabla hajaiingiza katika chombo mara tatu, kwani hakika mmoja wenu hajui ni wapi ulilala mkono wake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
8. Atakapoingia mtu nyumbani kwake, akamtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu wakati wa kuingia kwake na wakati wa kula kwake husema shetani kuwaambia jamaa zake: Hamna malazi wala chakula cha usiku kwenu, na atakapoingia akawa hakumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu wakati wa kuingia kwake, shetani husema: mmepata malazi na chakula cha usiku - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
9. Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake; kwani hakika fitina ya kwanza ya wana wa Israeli ilikuwa kwa wanawake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
10. Nilisali pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- rakaa mbili kabla ya adhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Ijumaa, na rakaa mbili baada ya magharibi, na rakaa mbili baada ya ishaa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
11. Paliletwa mashtaka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuhusu mtu anayepata wasiwasi kuwa anapata kitu ndani ya swala (katika vitenguzi vya udhu), Akasema: asiondoke mpaka asikie sauti, au apate harufu - 1 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
12. Hivi haogopi mmoja wenu anayenyanyua kichwa chake kabla ya imamu Mwenyezi Mungu kukigeuza kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye sura yake kuwa sura ya punda?
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
13. Alinifundisha mimi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- tashahudi (tahiyatu), mkono wangu ukiwa katikati ya mikono yake kama anavyonifundisha sura katika Qur'ani
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
14. Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiomba: Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na adhabu za kaburi, na adhabu ya moto, na mitihani ya uhai na kifo, na fitina za masihi dajali. - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
15. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na mashetani wa kiume na mashetani wa kike.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
16. Muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake msimshirikishe yeye na chochote, na acheni wanayosema baba zenu, na anatuamrisha swala na ukweli - 3 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
17. Hakika ukweli ni kwamba utakuja kutokea uchoyo baada yangu na mambo msiyoyajua(uzushi)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
18. Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapooga janaba, anaosha mikono yake kisha anatawadha udhu wake wa swala kisha anaoga
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
19. Je nisikuelezeni kwa kile ambacho ninakiogopea zaidi kwenu nyinyi kuliko hata masihi dajali? Wakasema: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: Ni shirki iliyofichikana, anasimama mtu kuswali anapendezesha swala yake kwakuwa anaona kuna mtu anamtazama - 1 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
20. Mfano wa aliyesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuingia ndani yake, ni kama mfano wa watu waliotengeneza boti (safina) wakawa baadhi yao wako juu ya safina na wengine wako chini yake, na wakawa wale walioko chini yake wanapohitajia maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao - 8 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
21. Msilifanye kaburi langu kuwa sikukuu, wala nyumba zenu kuwa makaburi, na nitakieni rehma, kwani dua zenu hunifikia popote mlipo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
22. Nilikuwa ni mtu mwenye madhii mengi, nikaona haya kumuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwasababu ya nafasi ya binti yake kwangu, nikamtuma Mikidadi bin Aswadi akamuuliza, akasema: Ataosha tupu yake, na atatawadha
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
23. Msiseme: Ni matakwa ya Mwenyezi Mungu na matakwa ya fulani, lakini semeni: Ni matakwa ya Mwenyezi Mungu kisha akataka fulani
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
24. Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, Hamtoingia peponi mpaka muamini, na hamtoamini mpaka mpendane, je nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? toleaneni salamu kwa wingi kati yenu. - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
25. Nilimuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni (kuiswali) swala kwa wakati wake. Nikasema: kisha nini? Akasema: Ni kuwatendea wema wazazi wawili - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
26. Yakwamba mtu mmoja alikula kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa mkono wake wa kushoto, akasema: kula kwa mkono wako wa kulia, akasema: siwezi. akasema: Hutoweza, hakuna kilichomzuia isipokuwa ni kiburi, basi hakuweza tena kuunyanyua kufika kinywani kwake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
27. Atakayelingania katika uongofu, atakuwa kwake kapata malipo mfano wa malipo ya aliyemfuata, halipunguzi hilo chochote katika malipo yao, na atakayelingania katika upotofu atakuwa kwake na madhambi mfano wa madhambi ya yule aliyemfuata, halipunguzi hilo katika madhambi yao chochote
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
28. Mikosi ya ndege ni shirki, na hakuna yeyote miongoni mwetu ispokuwa (ana chembe ya hilo), lakini Mwenyezi Mungu huliondoa kwa kumtegemea
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
29. Nilitoka katika kundi la Bani Aamir kwenda kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- tukasema: Wewe ni bwana wetu, basi akasema Bwana ni Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
30. Tahadharini na kuchupa mipaka, bila shaka kilichowaangamiza waliokuwa kabla yenu ni kuchupa mipaka
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
31. Kilipomfikia Abuu Twalib kifo, Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alimuendea akamkuta Abdullahi bin Abii Umaiyya na Abuu Jahli wakiwa wake, Akasema kumwambia mgonjwa: Ewe baba mdogo, Sema Laa ilaaha illa llaah -Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu-, neno ambalo nitakutetea kwalo kwa Mwenyezi Mungu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
32. Hakuna kuambukizana maradhi, wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, na kinachonipendeza zaidi ni kujipa matumaini. Wakasema: Ni nini matumaini? Akasema: Ni neno jema
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
33. Nikuwa yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- Alisema kuhusu maanswari (waliowapokea maswahaba waliohama kutoka Makka): Hawapendi mtu ila muumini, na hawachukii ila mnafiki, atakayewapenda Answaar na Mwenyezi Mungu atampenda, na atakayewachukia Mwenyezi Mungu atamchukia
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
34. Nilimshuhudia Amru bin Abii Hasan alimuuliza Abdullah bin Zaidi kuhusu udhu wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akaagiza bakuli la maji, akatawadha kwaajili yao udhu wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
35. Hakika inakutosheleza kusema kwa mikono yako hivi: kisha akapiga kwa mikono yake miwili chini ya ardhi mpigo mmoja, kisha akapaka mkono wa kulia kwa kutumia mkono wa wa kushoto, na akapaka juu ya viganja vyake na uso wake.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
36. Nilikuwa nikioga mimi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chombo kimoja sisi wote tukiwa na janaba
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
37. Atakayesema: -Yaani: anapotoka nyumbani kwake-: Bismillaahi tawakkaltu a'la llaahi -kwa jina la Mwenyezi Mungu nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Laa haulaa walaa quwwata illaa billaa- hakuna ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, huambiwa: Umeongozwa na umetoshelezwa na umekingwa, na shetani hujitenga mbali naye - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
38. Nilimpa utiifu Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- juu ya kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kumnasihi kila muislamu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
39. Mcheni Mwenyezi Mungu na mswali swala zenu tano, na mfunge mwezi wenu, na mtekeleze zaka za mali zenu, na muwatii viongozi wenu, mtaingia pepo ya Mola wenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
40. Adhabu kali ya moto itazipata nyayo za miguu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
41. Atakayependezwa na kumtazama mtu miongoni mwa watu wa peponi basi na amtazame huyu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
42. Mambo kumi ni katika maumbile: Kupunguza masharubu, na kuziachia ndevu,na kupiga mswaki, na kupandisha maji puani, na kupunguza kucha, na kuosha fundo za vidole, na kunyofoa nywele za makwapani, na kunyoa nywele za sehemu za siri, na kustanji kwa maji. - 8 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
43. Umma wangu wote watasalimika isipokuwa wenye kuyatangaza (madhambi) - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
44. Tulikuwa kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- watu tisa au nane au saba, akasema: Hivi hamumpi ahadi ya utiifu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
45. Nimeamrishwa nipambane na watu mpaka washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na wasimamishe swala, na watoe zaka, pindi watakapofanya hivyo watakuwa wamezikinga kutokana nami damu zao na mali zao isipokuwa kwa haki ya uislamu na hesabu yao itakuwa juu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
46. Amsalimie aliyepanda anayetembea, na anayetembea aliyekaa, na wachache kwa wengi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
47. Swala ya mtu katika jamaa inazidi swala yake sokoni kwake na nyumbani kwake kwa daraja zaidi ya ishirini
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
48. Hautonyanyuka unyayo wa mja siku ya Kiyama mpaka aulizwe kuhusu umri wake aliumaliza katika mambo yapi? Na kuhusu elimu yake aliifanyia kazi katika nini? Na kuhusu mali yake ni wapi aliichuma? Na aliitoa katika mambo gani? Na kuhusu mwili wake aliumaliza katika mambo yapi?
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
49. Hebu nielezeni lau kama Mto ungelikua mlangoni kwa mmoja wenu akioga humo kila siku mara tano, unasemaje kuhusu hilo, kunaweza kubaki na uchafu katika mwili wake?
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
50. Mfano wa waumini katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao na kufanyiana kwao upole, ni kama mfano wa kiwiliwili, kinapopata tabu kiungo kimoja vinaitana kwa ajili ya hicho kimoja viungo vyote kwa kukesha na maumivu - 6 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
51. Waamrisheni watoto wenu kuswali nao wakiwa watoto wa miaka saba, na wapigeni kwa ajili yake nao wakiwa watoto wa miaka kumi, na watenganisheni baina yao katika malazi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
52. Hakuna kitu chenye uzito zaidi katika mizani ya muumini siku ya Kiyama kuliko tabia njema, na hakika Mwenyezi Mungu anamchukia mtu muovu mwenye kauli chafu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
53. Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitoka kwetu sisi, tukasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumekwishafahamu ni vipi tutakusalimu, sasa ni vipi tutakutakia Rehema? - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
54. Hana swala yeyote ambaye hakusoma sura kifunguzi cha kitabu (suratul faatiha) - 4 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
55. Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Mwenyezi Mungu kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri,
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
56. Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mazuri, na Akhera mazuri, na utukinge na adhabu ya moto
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
57. Bwana wa Istighfari (Dua ya kuomba msamaha) - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
58. Ogopeni dhulma, kwa hakika dhulma ni giza siku ya kiyama. Na ogopeni tamaa, kwa hakika tamaa iliwaangamiza walio kuwepo kabla yenu - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
59. Ya kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani zimfikie: Ni Uislamu upi bora? Akasema: "Ni, ulishe chakula, na utoe salamu kwa unayemjua na usiyemjua
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
60. Kila mmoja miongoni mwenu ni mchunga hivyo ataulizwa kuhusu raia wake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
61. Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
62. Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zimfikie, akamsemesha katika baadhi ya mambo, akasema: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka, akasema Mtume rehema na amani zimfikie: "Umenifanya mimi kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu? sema: Akitaka Mwenyezi Mungu pekee
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
63. Watu wenye adhabu kali zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, ni wale wenye kutengeneza mfano wa vile alivyoviumba Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
64. Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
65. Sema: Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiyekuwa na mshirika, Mwenyezi Mungu mkubwa mno, na kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu kwa wingi, na ametakasika Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu, na hapana ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu mwenye nguvu na hekima - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
66. Hakuna Muislamu yeyote atafikiwa na Sala ya lazima kisha akaufanya vizuri udhu wake, na Unyenyekevu wake na Rakaa zake, isipokuwa inakuwa ni kifuta madhambi yaliyo kuwa kabla ya Sala, kwa muda ambao hajafanya madhambi makubwa, na hivyo ndivyo ilivyo kila siku
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
67. Mfano wa muumini mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa chenza harufu yake nzuri na ladha yake nzuri, na mfano wa muumini ambaye hasomi Qur'ani ni kama mfano wa tende: haina harufu na ladha yake ni tamu - 6 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
68. Adh-kari za baada ya sala ya faradhi hapati hasara msomaji au mfanyaji wake, kusema Sub-haana llahi mara thelathini na tatu (33), Al-hamdulillahi mara thelethini na tatu (33), Allahu Akbaru mara thelathini na nne (34)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
69. Atakayesema wakati anamsikia muadhini: Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Muhammadi kuwa ni Mtume na Uislamu kuwa ni dini, atasamehewa dhambi zake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
70. kanipinga mwanadamu na hakustahiki kufanya hivyo, na amenitukana na hakustahiki kufanya hivyo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
71. Atakayemfanyia uadui kipenzi changu basi nitakuwa nimemtangazia vita, na hatojiweka karibu kwangu mja kwa kitu ninachokipenda katika vile nilivyomfaradhishia juu yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
72. Atakayetundika hirizi atakuwa kafanya ushirikina
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
73. Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo saizi ya kucha miguuni kwake, akaiona Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: "Rudi katawadhe vizuri udhu wako" Akarudi, kisha akaswali
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
74. Aina mbili za watu ni miongoni mwa watu wa motoni, sijawaona (katika zama zake Mtume), watu walio na mijeledi mithili ya mikia ya Ng'ombe wakiwapiga watu, na wanawake waliovaa na wako uchi, wanenguaji wakatikaji
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
75. Asiangalie mwanaume katika uchi wa mwanaume mwenzie, wala mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
76. Hawafuatani Malaika na jamaa ambao ndani yao kuna mbwa au kengele
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
77. Tulikuwa hatuchukulii maji maji ya kahawia na njano baada ya twahara kuwa ni chochote
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
78. Kaa kiasi cha siku ambazo ilikuwa ikidumu hedhi yako, kisha oga
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
79. Kuoga siku ya Ijumaa ni wajibu kwa kila aliyebaleghe, na apige mswaki, na aguse marashi ikiwa atapata - 4 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
80. Muislamu wa kweli ni yule wanayepata Amani waislamu wenzake kutokana na ulimi wake na mkono wake, na mhamaji ni yule mwenye kuyahama yale aliyoyakataza Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
81. Asisafiri mwanamke mwendo wa siku mbili mpaka awe pamoja na mume wake, au maharimu yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa