1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti

Hadithi Nilikuwa nikioga mimi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chombo kimoja sisi wote tukiwa na janaba, na alikuwa akiniamrisha najifunga kikoi (kishida), ananigusa na mimi nikiwa katika hedhi

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤمنينَ رضي الله عنها قَالَتْ:

كُنْتُ أَغْتَسِلُ أَنَا وَالنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ إِنَاءٍ وَاحِدٍ كِلاَنَا جُنُبٌ، وَكَانَ يَأْمُرُنِي، فَأَتَّزِرُ، فَيُبَاشِرُنِي وَأَنَا حَائِضٌ، وَكَانَ يُخْرِجُ رَأْسَهُ إِلَيَّ وَهُوَ مُعْتَكِفٌ فَأَغْسِلُهُ وَأَنَا حَائِضٌ.

Imepokewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Nilikuwa nikioga mimi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chombo kimoja sisi wote tukiwa na janaba, na alikuwa akiniamrisha najifunga kikoi (kishida), ananigusa na mimi nikiwa katika hedhi, na alikuwa akitoa kichwa chake kwangu, naye akiwa katika itikafu (msikitini), ninamuosha nami nikiwa katika hedhi".

Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Swahiih Al Bukhaariy - 299

Ufafanuzi

Ameeleza Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu baadhi ya hali zake maalum pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na miongoni mwake: Nikuwa alikuwa akioga kutokana na janaba pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika chombo kimoja wakichota wote kwa pamoja. Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kumwendea akiwa katika hedhi anamuamrisha afunike mwili wake kuanzia kitovuni mpaka magotini, kisha akimshikashika bila ya tendo la ndoa. Nakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikaa itikafu msikitini anatoa kichwa chake kwa Aisha anamuosha naye akiwa nyumbani kwake na akiwa katika siku zake.

Katika Faida za Hadithi

  1. Inafaa mtu kuoga na mke wake katika chombo kimoja.
  2. Inafaa kumpapasa mwenye hedhi, mahali pasipokuwa tupu, nakuwa mwili wake ni twahara na wala si najisi.
  3. Inapendeza kwa mwanamke kuvaa kikoi (au mtandio) wakati wa kupapaswa.
  4. Kuchukua sababu zinazozuia kuingia katika haramu.
  5. Katazo kwa mwenye hedhi kukaa msikitini.
  6. Uhalali kwake wa kuvipapasa vitu vibichi au vikavu, ikiwemo kuziosha nywele na kuzitana
  7. Muamala mzuri wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa familia yake.

Kuonyesha Tafsiri

59 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
YO Yorùbá اليوروبا
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
SO Soomaali الصومالية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
CS Čeština التشيكية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
IT Italiano الإيطالية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
AZ Azərbaycan الأذربيجانية
UZ O‘zbek الأوزبكية
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
KMR Kurmancî الكرمنجية
Aina tofauti tofauti