«أَمَا يَخْشَى أَحَدُكُمْ - أَوْ: لاَ يَخْشَى أَحَدُكُمْ - إِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ قَبْلَ الإِمَامِ، أَنْ يَجْعَلَ اللَّهُ رَأْسَهُ رَأْسَ حِمَارٍ، أَوْ يَجْعَلَ اللَّهُ صُورَتَهُ صُورَةَ حِمَارٍ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Hivi haogopi mmoja wenu anayenyanyua kichwa chake kabla ya imamu Mwenyezi Mungu kukigeuza kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye sura yake kuwa sura ya punda?".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Hakika amewekwa imamu ndani ya swala ili afuatwe na aikamilishe, kiasi kwamba kufanyike kuhama kwa maamuma baada ya kuhama kwa imamu, na kwa hili kunathibiti kumfuata, maamuma akimtangulia, lengo linalotakiwa la kuwepo kwa imamu litakuwa limekosekana, ndio maana imekuja ahadi hii ya adhabu kali kwa mwenye kunyanyua kichwa chake kabla ya imamu wake, kwa Mwenyezi Mungu kukifanya kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye sura yake kuwa sura ya punda, kiasi kwamba aifute sura yake kutoka katika sura nzuri kuwa sura mbaya, ikiwa ni malipo kwa hiki kiungo ambacho kimenyanyuka na kuharibu swala.