1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti

Hadithi Mfano wa aliyesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuingia ndani yake, ni kama mfano wa watu waliotengeneza boti (safina)

عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:

«مَثَلُ القَائِمِ عَلَى حُدُودِ اللَّهِ وَالوَاقِعِ فِيهَا، كَمَثَلِ قَوْمٍ اسْتَهَمُوا عَلَى سَفِينَةٍ، فَأَصَابَ بَعْضُهُمْ أَعْلاَهَا وَبَعْضُهُمْ أَسْفَلَهَا، فَكَانَ الَّذِينَ فِي أَسْفَلِهَا إِذَا اسْتَقَوْا مِنَ المَاءِ مَرُّوا عَلَى مَنْ فَوْقَهُمْ، فَقَالُوا: لَوْ أَنَّا خَرَقْنَا فِي نَصِيبِنَا خَرْقًا وَلَمْ نُؤْذِ مَنْ فَوْقَنَا، فَإِنْ يَتْرُكُوهُمْ وَمَا أَرَادُوا هَلَكُوا جَمِيعًا، وَإِنْ أَخَذُوا عَلَى أَيْدِيهِمْ نَجَوْا، وَنَجَوْا جَمِيعًا».

Kutoka kwa Nuumaan bin bashiri Radhi za Allah ziwe juu yao, kutoka kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Mfano wa aliyesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuingia ndani yake, ni kama mfano wa watu waliotengeneza boti (safina), wakawa baadhi yao wako juu ya safina na wengine wako chini yake, na wakawa wale walioko chini yake wanapohitajia maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao, wakasema: Lau kama tungetoboa katika sehemu yetu kitobo wala tusingewaudhi walioko juu yetu, ikiwa watawaacha watekeleze walilolikusudia wataangamia wote, na ikiwa watawashika na kuwazuia wataokoka na wataokoka wote".

الملاحظة
رائع
النص المقترح لا يوجد...
الملاحظة
التفسير مطول جدآ وغير مفهوم أنه مبهم للغايه
النص المقترح لماذا التفسير مطول للغايه ؟

Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy Swahiih Al Bukhaariy - 2493

Ufafanuzi

Mtume Rehema na amani ziwe juu yake amepiga mfano wa wale wenye kusimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu, wenye msimamo katika amri ya Mwenyezi Mungu, wenye kuamrisha mema na kukataza maovu, na mfano wa wenye kutumbukia katika mipaka ya Mwenyezi Mungu wenye kuacha mema, na kufanya maovu, na athari ya hilo katika kusalimika jamii, ni sawa na mfano wa watu waliopanda boti, wakagawana nafasi nani akae juu na nani akae chini ya boti, wengine wakapata nafasi ya kukaa juu na wengine wakapata nafasi ya kukaa chini, na wakawa hawa walioko chini wanapotaka kuchota maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao, Kisha wale wa chini wakasema: Lau tungeli toboa tundu mahali petu chini ili tusiwaudhi walio juu yetu, basi lau walio juu wangewaacha kufanya hivyo, basi meli ingewazamisha wote, na lau wangeliwakataza na kuwazuia, makundi yote mawili yangeokoka.

الملاحظة
الشدة مكررة مرتين عند كلمة النبي
النص المقترح لا يوجد...

Katika Faida za Hadithi

  1. Umuhimu wa kuamrisha mema na kukataza maovu katika kuzihifadhi jamii na kusalimika kwake.
  2. Miongoni mwa njia ya ufundishaji ni kupiga mifano, kwa ajili ya kusogeza uelewa wa akili kwa picha ya kitu chenye kueleweka.
  3. Kufanya uovu kwa wazi na kuto kukemea madhara yake yanarudi katika jamii nzima.
  4. Kuangamia kwa jamii kunaambatana na kuwaacha waovu wakiendelea kutapakaza maovu katika Ardhi.
  5. Kufanya mambo kimakosa na nia ikawa njema hili halitoshi kurekebisha matendo.
  6. Majukumu katika jamii ya kiislamu ni ya watu wote, hayaegemezwi kwa mtu maalum.
  7. Kuadhibiwa kwa watu wote kwa sababu ya madhambi ya wachache, ikiwa hayatokemewa.
  8. Waovu hudhihirisha maovu yao kwa sura ya kheri katika jamii kama walivyo wanafiki.

Kuonyesha Tafsiri

58 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
YO Yorùbá اليوروبا
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
SO Soomaali الصومالية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
CS Čeština التشيكية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
AZ Azərbaycan الأذربيجانية
UZ O‘zbek الأوزبكية
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
KMR Kurmancî الكرمنجية
Aina tofauti tofauti
  • . .