انْطَلَقْتُ في وَفدِ بَنِي عَامِرٍ إِلى رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم، فَقُلنا: أَنتَ سيّدُنَا، فقال: «السَّيدُ اللهُ»، قُلنا: وَأَفْضَلُنا فَضْلاً، وأعظَمُنا طَوْلاً، فقال: «قُولُوا بِقَولِكُم، أَو بَعضِ قولِكُم، وَلَا يَسْتَجْرِيَنَّكُم الشَّيطَانُ».
[صحيح] - [رواه أبو داود وأحمد]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdillahi bin Shikh-khir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: "Nilitoka katika kundi la Bani Aamir kwenda kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- tukasema: Wewe ni bwana wetu, basi akasema Bwana ni Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka-. Tukasema: Na mbora wetu kwa fadhila na mtukufu wetu katika uwezo. Basi akasema: semeni kwa kauli zenu au baadhi ya kauli zenu, na wala asikufanyeni shetani kuwa wawakilishi wake".
Sahihi - Imepokelewa na Abuu Daud
Lilipopitiliza na kuzidisha kundi hili katika kumsifia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Aliwakataza kuhusu hilo; kwaajili ya kuwa na adabu na Mwenyezi Mungu -Mtukufu- na kwa kuilinda Tauhidi, na akawaamrisha waishie katika matamshi ambayo hayana kuvuka mipaka ndani yake wala makatazo, kama kumuita Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kama alivyomuita Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka-, au Nabii wa Mwenyezi Mungu, au baba Qassim, na akawatahadharisha asijekuwafanya shetani kuwa ni mawakala wake katika matendo anayowatia wasiwasi kwao.