عَنْ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:

«إِنَّ اللهَ عَزَّ وَجَلَّ يَنْهَاكُمْ أَنْ تَحْلِفُوا بِآبَائِكُمْ»، قَالَ عُمَرُ: فَوَاللهِ مَا حَلَفْتُ بِهَا مُنْذُ سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى عَنْهَا ذَاكِرًا وَلَا آثِرًا.
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Omar bin Khattwabi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni msije kuapa (kupitia) kwa baba zenu". Na kwa Imamu Muslim: "Atakayetaka kuapa basi na aape kwa jina la Mwenyezi Mungu au anyamaze". Na katika riwaya nyingine Amesema Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Namuapa Mwenyezi Mungu, sijawahi kuapa kwa kiapo hicho tena tangu nilipomsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akikikataza, nikikitaja mwenyewe au nikinukuu cha mtu mwingine"
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Alimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akiwa anaapa kwa baba yake, akamkataza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- tena kwa kunyanyua sauti yake: "Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni msiape (kupitia) kwa baba zenu" wakaitekeleza maswahaba amri ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na wakawa hawaapi tena ila kwa jina la Mwenyezi Mungu, mpaka akaeleza Omar kuwa yeye hakuapa tena kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu tangu alipomsikia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akikataza hilo, si kwa kukusudia wala kwa kunukuu kiapo cha mwingine aliyeapa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Maana ya Maneno

ذاكِرًا:
عامِدًا.
آثِرًا:
حاكِيًا عن غَيْرِي أنَّه حَلَفَ بها.
Ziada