1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti

Hadithi Hakika utakuja kutokea uchoyo na kujipendelea baada yangu na mambo msiyoyajua (uzushi)" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu unatuamrisha nini? Akasema: "Mtekeleze haki ya wajibu kwenu, na mumuombe Allah haki yenu

عَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:

«سَتَكُونُ أَثَرَةٌ وَأُمُورٌ تُنْكِرُونَهَا» قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ فَمَا تَأْمُرُنَا؟ قَالَ: «تُؤَدُّونَ الحَقَّ الَّذِي عَلَيْكُمْ، وَتَسْأَلُونَ اللَّهَ الَّذِي لَكُمْ».

Imepokelewa kutoka kwa Bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Hakika utakuja kutokea uchoyo na kujipendelea baada yangu na mambo msiyoyajua (uzushi)" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu unatuamrisha nini? Akasema: "Mtekeleze haki ya wajibu kwenu, na mumuombe Allah haki yenu".

Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Swahiih Al Bukhaariy - 3603

Ufafanuzi

Alieleza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake yakuwa waislamu watatawaliwa na viongozi watakaohodhi na kujipendelea mali za waislamu na mambo mengine mengi yasiyokuwa mali, watazitumia kama watakavyo, na watawanyima waislamu haki yao katika mali hizo. Na watakuwa na mambo ndani ya dini mtakayoyakataa kuwa si katika dini. Masahaba Radhi za Allah ziwe juu yao wakauliza: Ni nini watafanya katika hali kama hiyo? Akawaeleza Rehema na amani ziwe juu yake kuwa kusikuzuieni kule kuhodhi kwao mali na kujipendelea kwao, nanyi mkaacha kufanya wajibu wenu kwao, ikiwemo usikivu na utii, bali kuweni na subira na mtii msiwaletee upinzani katika madaraka, na haki yenu iombeni kutoka kwa Allah, na awarekebishe na azuie shari zao na dhulma zao.

Katika Faida za Hadithi

  1. Hadithi hii ni katika dalili za utume wake Rehema na amani ziwe juu yake, kiasi ambacho alieleza mambo yatakayotokea ndani ya Umma wake na yakatokea kama alivyoeleza.
  2. Inafaa kumueleza mtahiniwa yale yatakayomsibu katika mitihani; ili aitulize nafsi yake, mtihani ukimfika atakuwa na subira na atataraji malipo toka kwa Allah.
  3. Kushikamana na Qur'ani na Sunna ni sababu ya kutoka katika fitina na hitilafu.
  4. Himizo la kuwa wasikivu na watiifu kwa viongozi katika mema, na kutojitoa katika utiifu, hata kama zitatokea kwao dhulma.
  5. Kutumia hekima na kufuata mafundisho ya Mtume wakati wa fitina.
  6. Ni jukumu la kila mtu kutimiza haki ya msingi inayomlazimu hata kama itatokea kadhulumiwa.
  7. Hadithi inaashiria kanuni ya msingi ambayo ni: Mtu kuchagua moja kati ya shari mbili au madhara yenye nafuu.

Kuonyesha Tafsiri

58 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
YO Yorùbá اليوروبا
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
SO Soomaali الصومالية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
CS Čeština التشيكية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
AZ Azərbaycan الأذربيجانية
UZ O‘zbek الأوزبكية
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
KMR Kurmancî الكرمنجية
Aina tofauti tofauti
  • . .