عَنْ أَبِي رُقَيَّةَ تَمِيمِ بْنِ أَوْسٍ الدَّارِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«الدِّينُ النَّصِيحَةُ» قُلْنَا: لِمَنْ؟ قَالَ: «لِلهِ وَلِكِتَابِهِ وَلِرَسُولِهِ وَلِأَئِمَّةِ الْمُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [الأربعون النووية: 7]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ruqaiyya Tamim Ausi Ad-dari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Dini ni nasaha" Tukasema: Kwa ajili ya nani? Akasema: "Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kitabu chake, na Mtume wake, na kwa viongozi wa waislamu na watu wote."
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [الأربعون النووية - 7]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa dini imesimama katika msingi wa utakasifu wa nia na ukweli, ili itekelezwe kama alivyowajibisha Mwenyezi Mungu kikamilifu pasina mapungufu au udanganyifu. Pakasemwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Zinakuwa kwa nani nasaha? Akasema: Kwanza: Nasaha ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka: Kwa kutakasa matendo kwa ajili yake, na kutomshirikisha, na tuamini ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, na kutukuza amri zake, na kuwaita watu kuja katika kumuamini. Pili: Nasaha kwa ajili ya kitabu chake ambacho ni Qur'ani tukufu: Tuitakidi kuwa ni maneno yake, na ni kitabu chake cha mwisho, na kwamba kimefuta sheria zote zilizokuwa kabla yake, na tunakitukuza na kukisoma haswa ipasavyo, na tunazifanyia kazi aya zake,zilizo wazi na tunazikubali zenye kutatiza na tunapingana na tafsiri mbaya ya wenye kuzipotosha, na tunachukua mazingatio kwa mawaidha yake, na kuisambaza elimu yake, na kuwalingania watu kwayo. Tatu: Nasaha kwa ajili ya Mtume wake Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake: Kwa sisi kuitakidi kuwa yeye ni mwisho wa Mitume, na kumuamini kwa yale aliyokuja nayo, na tutekeleza amri yake, na tuepuke makatazo yake, na tusimuabudu Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa yale aliyokuja nayo, na tunaitukuza na tunaiheshimu, na tunautangaza ujumbe wake, na kuisambaza sheria yake, na kupinga tuhuma zote dhidi yake. Nne: Nasaha kwa viongozi wa Waislamu: Kwa kuwasaidia katika haki, na kutozozana nao katika uongozi, na kuwasikiliza na kuwatii katika kumtii Mwenyezi Mungu. Tano: Nasaha kwa Waislamu: Kwa kuwatendea wema na kuwalingania, na kuacha kuwaudhi, na kuwapendelea heri, na kusaidizana nao katika wema na uchamungu.