عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ صَخْرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْت رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم يَقُولُ:
«مَا نَهَيْتُكُمْ عَنْهُ فَاجْتَنِبُوهُ، وَمَا أَمَرْتُكُمْ بِهِ فَافْعَلُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ، فَإِنَّمَا أَهْلَكَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ كَثْرَةُ مَسَائِلِهِمْ، وَاخْتِلَافُهُمْ عَلَى أَنْبِيَائِهِمْ».
[صحيح] - [رواه البخاري ومسلم] - [الأربعون النووية: 9]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira Abdul-Rahman bin Swakhar -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Yale niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi fanyeni katika hayo kadiri muwezavyo, na hakika waliangamia wale waliokuwa kabla yenu, kwa kukithiri maswali yao, na kuhitilafiana kwao na Manabii wao".
-
Ametubainishia sisi Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa atakapotukataza kitu basi ni wajibu juu yetu kukiacha pasina kubagua, na atakapotuamrisha kwa chochote basi ni juu yetu kukifanya kile tunachokiweza. Kisha akatutahadharisha ili tusije kuwa kama baadhi ya umma zilizopita pindi walipokithirisha maswali juu ya Manabii wao ikiwa ni pamoja na kwenda kinyume nao, basi Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa aina mbali mbali za maangamivu na uharibifu, tunatakiwa tusiwe mfano wao ili tusiangamie kama walivyoangamia.