عَنِ ابْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:

«أُمِرْتُ أَنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى يَشْهَدُوا أَنْ لاَ إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ، وَيُقِيمُوا الصَّلاَةَ، وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ، فَإِذَا فَعَلُوا ذَلِكَ عَصَمُوا مِنِّي دِمَاءَهُمْ وَأَمْوَالَهُمْ إِلَّا بِحَقِّ الإِسْلاَمِ، وَحِسَابُهُمْ عَلَى اللَّهِ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Omari bin Khattwab na mwanaye Abdillahi na Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Nimeamrishwa nipambane na watu mpaka washuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na wasimamishe swala, na watoe zaka, pindi watakapofanya hivyo watakuwa wamezikinga kutokana nami damu zao na mali zao isipokuwa kwa haki ya uislamu na hesabu yao itakuwa juu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu".
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim katika riwaya zake zote

Ufafanuzi

Hakika Mwenyezi Mungu ameamrisha kupigana na washirikina mpaka washuhudie kuwa hakuna muabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika, na washuhudie kuwa Muhammadi ana utume, na wayafanyie kazi yanayotakiwa katika shahada hii ikiwa ni pamoja na kudumu na swala tano, na zaka inapolazimu, pindi watakaposimamisha nguzo hizi pamoja na yale aliyowawajibishia Mwenyezi Mungu juu yao, basi watakuwa wamezuia na wamehifadhi damu yao kutokuuwawa, na mali zao kwasababu ya kuzilinda kwa uislamu, isipokuwa kwa haki ya uislamu, kwa kutokea toka kwa mmoja wao lile litakalopelekea sheria ya uislamu kumchukulia hatua kama kisasi au kusimamishiwa sheria au mengineyo, na atakayeyafanya yale aliyoamrishwa basi huyo ni muumini, na atakayefanya kwa kujikinga na kuhofia juu ya mali yake na damu yake basi huyo ni mnafiki, na Mwenyezi Mungu anayajua yale anayoyaficha na atamuhesabu juu yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Maana ya Maneno