1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti

Hadithi Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zimfikie, akamsemesha katika baadhi ya mambo, akasema: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka, akasema Mtume rehema na amani zimfikie: "Umenifanya mimi kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu? sema: Akitaka Mwenyezi Mungu pekee

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما:

أَنَّ رَجُلًا أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَكَلَّمَهُ فِي بَعْضِ الْأَمْرِ، فَقَالَ: مَا شَاءَ اللهُ وَشِئْتَ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَجَعَلْتَنِي لِلَّهِ عَدْلًا؟ قُلْ: مَا شَاءَ اللهُ وَحْدَهُ».

Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-:
Yakwamba mtu mmoja alikuja kwa Mtume rehema na amani zimfikie, akamsemesha katika baadhi ya mambo, akasema: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka, akasema Mtume rehema na amani zimfikie: "Umenifanya mimi kuwa mshirika wa Mwenyezi Mungu? sema: Akitaka Mwenyezi Mungu pekee".

Upokezi wake ni mzuri Imepokelewa na Nasai katika Sunan Alkubra na Ibn Majah na Ahmad Sunan Alkubraa cha Imam Nasai - 10759

Ufafanuzi

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani zimfikie akamsemesha kuhusu jambo lake binafsi, kisha akasema: "Akitaka Mwenyezi Mungu na ukataka wewe", Mtume rehema na amani zimfikie akaikemea kauli hii, na akamueleza kuwa kuunganisha matashi ya kiumbe na matashi ya Mwenyezi Mungu kwa kiunganishi "na" ni shirki ndogo, haifai kwa muislamu kuitamka, kisha akamuelekeza katika kauli ya sawa na ya haki: "Akitaka Mwenyezi Mungu peke yake", ampwekeshe Mwenyezi Mungu katika matashi, na wala asiunganishe matashi ya yeyote kwa aina yoyote ya kiunganishi.

Katika Faida za Hadithi

  1. Katazo la kusema: Akitaka Mwenyezi Mungu na ukitaka, na mfano wake katika yale yanayounganisha matashi ya mja katika matashi ya Mwenyezi Mungu kwa "na"; kwani hii ni katika shirki ndogo.
  2. Ulazima wa kukemea uovu.
  3. Mtume rehema na amani zimfikie alilinda mipaka ya tauhidi, na akaziba njia za ushirikina.
  4. Wakati wa kuondoa uovu ni vyema kumuelekeza anayefikishiwa ujumbe katika mbadala wa halali, kwa kumuiga Mtume rehema na amani zimfikie.
  5. Kukusanya baina ya kauli yake rehema na amani zimfikie katika hadithi hii: "Akitaka Mwenyezi Mungu peke yake", na kauli yake katika hadithi nyingine: "Sema: Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka wewe" Nikuwa kauli ya mtu: " Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka wewe", hii inafaa, lakini kauli ya: "Akitaka Mwenyezi Mungu peke yake" ndio bora zaidi.
  6. Inafaa kusema: "Akitaka Mwenyezi Mungu kisha ukitaka" lakini bora zaidi ni kusema: "Akitaka Mwenyezi Mungu pekee".

Kuonyesha Tafsiri

58 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
YO Yorùbá اليوروبا
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
SO Soomaali الصومالية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
CS Čeština التشيكية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
IT Italiano الإيطالية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
AZ Azərbaycan الأذربيجانية
UZ O‘zbek الأوزبكية
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
KMR Kurmancî الكرمنجية
Aina tofauti tofauti