«إِذَا سَمِعْتُمُ النِّدَاءَ، فَقُولُوا مِثْلَ مَا يَقُولُ المُؤَذِّنُ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudriy Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Amesema Mtume Rehema na Amani zimfikie: "Mtakapomsikia muadhini basi semeni mfano wa jinsi anavyosema".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Mtakapomsikia muadhini kwaajili ya swala basi mjibuni, kwa kusema mfano wa anayoyasema, sentensi kwa sentensi,na anaposema Allahu Akbaru semeni Allahu Akbaru, na anapoleta shahada mbili basi zileteni baada yake, kwani zitapatikana kwenu thawabu zile zilizokupiteni katika thawabu za kuadhini alizojikusanyia muadhini, na Mwenyezi Mungu ni mpana wa vipawa, mwenye kujibu dua. Linaondolewa katika hadithi tamko la (Haiyya a'lasswalaa, Haiyya a'lal falaah) kwani hapo atasema baada yake: Laa haulaa walaa quwwata illaa billa- Hapana ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu.