1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti

Hadithi Nilimpa ahadi ya utiifu Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kusikia na kutii, na nasaha kwa kila muislamu

عَنْ جَرِيرِِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رضي الله عنه قَالَ:

بَايَعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى شَهَادَةِ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ، وَإِقَامِ الصَّلاَةِ، وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ، وَالنُّصْحِ لِكُلِّ مُسْلِمٍ.

Imepokelewa kutoka kwa Jariri Bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Nilimpa ahadi ya utiifu Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kusikia na kutii, na nasaha kwa kila muislamu.

Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Swahiih Al Bukhaariy - 2157

Ufafanuzi

Anaeleza swahaba Jariiri Bin Abdallah radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye alishikamana na maamrisho na akampa ahadi Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kutekeleza swala tano za faradhi usiku na mchana, kwa kutimiza sharti zake na nguzo zake na wajibu zake na sunna zake, na kutelekeza zaka ya wajibu, nayo ni ibada ya mali ya lazima, huchukuliwa toka kwa matajiri na kupewa wanaostahiki katika mafakiri na wengineo, na kuwatii viongozi, na kumpa nasaha kila muislamu, na hii ni kwa kuchunga masilahi yake, na kumfikishia kheri, na kumkinga na shari kwa kauli na vitendo.

Katika Faida za Hadithi

  1. Umuhimu wa swala na zaka, nazo ni katika nguzo za Uislamu.
  2. Umuhimu wa nasaha na kunasihiana kati ya waislamu, mpaka wakampa ahadi ya utiifu Masahaba radhi za Allah ziwe juu yake Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Kuonyesha Tafsiri

58 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
YO Yorùbá اليوروبا
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
SO Soomaali الصومالية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
CS Čeština التشيكية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
IT Italiano الإيطالية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
AZ Azərbaycan الأذربيجانية
UZ O‘zbek الأوزبكية
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
KMR Kurmancî الكرمنجية
Aina tofauti tofauti