1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti

Hadithi Hamtoingia peponi mpaka muamini, na hamtoamini mpaka mpendane, je nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? toleaneni salamu kwa wingi kati yenu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:

«لَا تَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّى تُؤْمِنُوا، وَلَا تُؤْمِنُوا حَتَّى تَحَابُّوا، أَوَلَا أَدُلُّكُمْ عَلَى شَيْءٍ إِذَا فَعَلْتُمُوهُ تَحَابَبْتُمْ؟ أَفْشُوا السَّلَامَ بَيْنَكُمْ».

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -sala na amani ziwe juu yake-:
"Hamtoingia peponi mpaka muamini, na hamtoamini mpaka mpendane, je nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? toleaneni salamu kwa wingi kati yenu".

Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim Swahiih Muslim - 54

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake yakuwa hatoingia peponi ila muumini, na wala haikamiliki imani na wala haitengemai hali ya jamii ya kiislamu mpaka wapendane baina yao. Kisha akaelekeza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake katika jambo muhimu zaidi ambalo litaleta mapenzi kwa wote, nalo ni waislamu kutoleana salam baina yao, aliyoifanya Mwenyezi Mungu kuwa ni salam kwa waja wake.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuingia peponi hakui ila kwa imani.
  2. Katika ukamilifu wa imani ni muislamu kumpendelea muislamu mwenzake yale anayoyapenda yeye.
  3. Ni sunna kutoa salam na kuisambaza kwa waislamu; kwa sababu kuisambaza ni kusambaza mapenzi na amani baina ya watu.
  4. Salam haitolewi ila kwa muislamu; kwa kauli yake Rehema na amani ziwe juu yake: "Baina yenu".
  5. Kutoa salam kunaondoa chuki na kuhamana na vifundo.
  6. Umuhimu wa mapenzi kati ya waislamu nakuwa hilo ni katika ukamilifu wa imani.
  7. Imekuja katika hadithi nyingine kuwa namna ya salam kamili ni: "As-salaam alaikum warahmatullahi wabarakaatuh", na inatosha: "Assalaam alaikum".

Kuonyesha Tafsiri

58 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
YO Yorùbá اليوروبا
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
SO Soomaali الصومالية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
CS Čeština التشيكية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
AZ Azərbaycan الأذربيجانية
UZ O‘zbek الأوزبكية
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
KMR Kurmancî الكرمنجية
Aina tofauti tofauti
  • .