1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti

Hadithi Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, alisema hivyo mara tatu", Na hakuna yeyote miongoni mwetu isipokuwa ana chembe ya hilo, isipokuwa Mwenyezi Mungu huliondoa kwa kumtegemea

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسعودٍ رضي الله عنه عن رَسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم قال:

«الطِّيَرَةُ شِرْكٌ، الطِّيَرَةُ شِرْكٌ، الطِّيَرَةُ شِرْكٌ، -ثلاثًا-»، وَمَا مِنَّا إِلَّا، وَلَكِنَّ اللهَ عَزَّ وَجَلَّ يُذْهِبُهُ بِالتَّوَكُّلِ.

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, Kuamini mikosi ni shirki, alisema hivyo mara tatu", Na hakuna yeyote miongoni mwetu isipokuwa ana chembe ya hilo, isipokuwa Mwenyezi Mungu huliondoa kwa kumtegemea.

Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad Sunanu Abii Daud - 3915

Ufafanuzi

Ametahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokana na imani ya mikosi: Nayo ni kuamini mikosi ya chochote chenye kusikika au chenye kuonekana, kama ndege au wanyama au walemavu au namba au siku au kinginecho, Na bila shaka ametaja ndege kwa sababu ndio ilikuwa maarufu kipindi cha zama za ujinga, na asili yake ni kumuachia ndege aruke katika jambo kama safari au biashara au kinginecho, akiruka pande wa kulia anajipa bishara na anatekeleza anachotaka kukifanya, na akirukia upande wa kushoto, anaamini ni mkosi na anaacha kufanya alichotaka kukifanya. Na akaeleza kuwa kitendo hicho ni ushirikina, na mikosi imekuwa ni ushirikina kwa sababu hakuna aletaye kheri ila Mwenyezi Mungu, na wala hazuii shari ila Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika.
Na ametaja bin Masoud radhi za Allah ziwe juu yake kuwa inaweza kuingia katika moyo wa muislamu kiasi kidogo cha imani ya mkosi, lakini anatakiwa akizuie kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, ikiwa ni pamoja na kufanya sababu.

Katika Faida za Hadithi

  1. Mikosi ni ushirikina; kwa sababu ndani yake kuna kuufungamanisha moyo kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu.
  2. Umuhimu wa kurudia mambo muhimu, ili yahifadhike na yakite ndani ya moyo.
  3. Mikosi huondolewa kwa kutegemea kwa Allah Mtukufu.
  4. Amri ya kutegemea kwa Allah pekee na moyo kufungamana naye Mtukufu.

Kuonyesha Tafsiri

58 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
YO Yorùbá اليوروبا
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
SO Soomaali الصومالية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
CS Čeština التشيكية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
AZ Azərbaycan الأذربيجانية
UZ O‘zbek الأوزبكية
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
KMR Kurmancî الكرمنجية
Aina tofauti tofauti
  • . . .
  • .