1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti

Hadithi Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake Alisema kuhusu maanswari (watu wa Madina): Hawampendi ila mtu muumini, na hawamchukii ila mnafiki, atakayewapenda Answaar na Mwenyezi Mungu atampenda, na atakayewachukia Mwenyezi Mungu atamchukia

عَنِ الْبَرَاءِ رضي الله عنه:

عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ فِي الْأَنْصَارِ: «لَا يُحِبُّهُمْ إِلَّا مُؤْمِنٌ، وَلَا يُبْغِضُهُمْ إِلَّا مُنَافِقٌ، مَنْ أَحَبَّهُمْ أَحَبَّهُ اللهُ وَمَنْ أَبْغَضَهُمْ أَبْغَضَهُ اللهُ».

Imepokelewa kutoka kwa Baraa -Radhi za Allah ziwe juu yake:
Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake Alisema kuhusu maanswari (watu wa Madina): Hawampendi ila mtu muumini, na hawamchukii ila mnafiki, atakayewapenda Answaar na Mwenyezi Mungu atampenda, na atakayewachukia Mwenyezi Mungu atamchukia".

Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Swahiih Muslim - 75

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa, kuwapenda Manswari katika watu wa Madina, ni alama ya ukamilifu wa imani; na hii ni kwa sababu ya kuwahi kwao kuutetea Uislamu na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kuleta amani pia, na kwenda kwao mbio kuwapa hifadhi waislamu, na kutoa kwao mali zao na nafsi zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, nakuwa kuwachukia ni alama ya unafiki. Kisha akaweka wazi -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayewapenda Manswari Mwenyezi Mungu humpenda, na atakayewachukia Mwenyezi Mungu humchukia.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuna nafasi kubwa ya Manswari, kuwapenda kwao ni alama ya imani na ni kujiweka mbali na unafiki.
  2. Kuwapenda vipenzi wa Mwenyezi Mungu na kuwatetea ni sababu ya Mwenyezi Mungu kumpenda mja.
  3. Fadhila na ubora wa wale waliotangulia katika Uislamu.

Kuonyesha Tafsiri

59 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
YO Yorùbá اليوروبا
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
SO Soomaali الصومالية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
CS Čeština التشيكية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
IT Italiano الإيطالية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
AZ Azərbaycan الأذربيجانية
UZ O‘zbek الأوزبكية
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
KMR Kurmancî الكرمنجية
Aina tofauti tofauti
  • .