1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti

Hadithi Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfanyie wema zaidi? Akasema: "Mama yako, kisha mama yako kisha mama yako, kisha baba yako, kisha anayefuata kwa ukaribu kisha anayemfuata kwa ukaribu

عَنْ بَهْزِ بْنِ حَكِيمٍ عَنْ أَبِيهِ عَنْ جَدِّهِ قَالَ:

قُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ: مَنْ أَبَرُّ؟ قَالَ: «أُمَّكَ، ثُمَّ أُمَّكَ، ثُمَّ أُمَّكَ، ثُمَّ أَبَاكَ، ثُمَّ الْأَقْرَبَ فَالْأَقْرَبَ».

Kutoka kwa Bahzi bin Hakim kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema:
Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani nimfanyie wema zaidi? Akasema: "Mama yako, kisha mama yako kisha mama yako, kisha baba yako, kisha anayefuata kwa ukaribu kisha anayemfuata kwa ukaribu".

Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ahmad Sunanu Abii Daud - 5139

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mtu muhimu zaidi kufanyiwa wema kuliko wote, na kumfanyia hisani, na kuamiliana naye vizuri, na kuishi naye vizuri, na kusuhubiana naye na kumuunga: Ni mama, na akasisitiza haki ya mama zaidi kuliko mtu mwingine, kwa kulirudia hilo mara tatu; kwa kubainisha fadhila zake kuliko watu wengine bila kupunguza chochote. Kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake anayefuata katika kutendewa wema: Kisha baba, kisha ndugu wa karibu zaidi na wa karibu anayefuata, kila ndugu anavyozidi kuwa karibu basi anakuwa na haki zaidi ya kuungwa udugu kuliko ndugu wa mbali.

Katika Faida za Hadithi

  1. Mazungumzo haya ni katika kumtanguliza mama, kisha baba, kisha ndugu wa karibu zaidi na wa karibu anayefuata, kulingana na daraja zao katika ukaribu.
  2. Kumebainishwa nafasi ya wazazi wawili na hasa hasa mama.
  3. Amekariri katika hadithi wema kwa mama mara tatu; na hii ni kwa sababu ya ukubwa wa fadhila yake kwa watoto wake, na kwa sababu ya wingi wa matatizo anayovumilia na tabu na uzito wa ujauzito, kisha kujifungua, kisha kunyonyesha, mambo ambayo yako kwake pekee, kisha baba anashiriki katika malezi.

Kuonyesha Tafsiri

43 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ID Indonesia الإندونيسية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
Aina tofauti tofauti