1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti

Hadithi Atakaye msabihi Mwenyezi Mungu mwisho wa kila swala mara thelathini na tatu (33), na akamhimidi Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu (33), na akamtukuza Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu, hizo ni tisini na tisa (99) Na akasema ili kukamilisha mia moja (100): Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul Mulku walahul hamdu, wahuwaa'laa kulli shai in qadiir, basi yatasamehewa madhambi yake, hata kama yalikuwa na wingi mfano wa povu la Bahari

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:

«مَنْ سَبَّحَ اللهَ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلَاةٍ ثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ، وَحَمِدَ اللهَ ثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ، وَكَبَّرَ اللهَ ثَلَاثًا وَثَلَاثِينَ، فَتْلِكَ تِسْعَةٌ وَتِسْعُونَ، وَقَالَ: تَمَامَ الْمِائَةِ: لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ غُفِرَتْ خَطَايَاهُ وَإِنْ كَانَتْ مِثْلَ زَبَدِ الْبَحْرِ».

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakaye msabihi Mwenyezi Mungu mwisho wa kila swala mara thelathini na tatu (33), na akamhimidi Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu (33), na akamtukuza Mwenyezi Mungu mara thelathini na tatu, hizo ni tisini na tisa (99) Na akasema ili kukamilisha mia moja (100): Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul Mulku walahul hamdu, wahuwaa'laa kulli shai in qadiir, basi yatasamehewa madhambi yake, hata kama yalikuwa na wingi mfano wa povu la Bahari".

Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim Swahiih Muslim - 597

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema baada ya kumalizika kwa swala za faradhi:
Mara thelathini na tatu (33): (Sub-haanallaah) Nako ni kumtakasa Mwenyezi Mungu dhidi ya mapungufu.
Na mara thelathini na tatu (33): (Alhamdulillaah) Nako ni kumsifu Mwenyezi Mungu kwa sifa kamilifu pamoja na kumpenda na kumtukuza.
Na mara thelathini na tatu (33): (Allaahu Akbar) Nayo ni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkuu na Mtukufu kuliko kila kitu.
Na kwa kukamilisha idadi ya mia moja (100) "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul Mulku, walahul hamdu, wahuwa alaa kulli shai in-Qadiir" Na maana yake: Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Yeye pekee asiye na mshirika, nakuwa Yeye Mtukufu ndiye alipwekeka kwa Ufalme kamilifu, na ndiye mwenye kustahiki kutukuzwa na sifa pamoja na mapenzi na kukwezwa pasina mwingine, nakuwa Yeye ni muweza hakuna kinachomshinda.
Yeyote atakayesema hivyo, dhambi zake zitafutwa na kusamehewa, hata zikiwa nyingi, kama povu jeupe litokalo juu ya bahari inapochafuka na kutibuka.

الملاحظة
ليتكم تزيدون في الشرح أن غفران الذنوب يُقصد بها الصغائر لأن بعض الناس قد يظن أنها تشمل الكبائر جزاكم الله خيرا
النص المقترح لا يوجد...

Katika Faida za Hadithi

  1. Sunna ya dhikiri hizi kuzisema baada ya swala za faradhi.
  2. Dhikiri hizi ni sababu ya kusamehewa madhambi.
  3. Ukubwa wa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu na rehema zake na msamaha wake.
  4. Dhikiri hii ni sababu ya kusamehewa madhambi, na kinachokusudiwa hapa ni: kufutiwa madhambi madogo, ama madhambi makubwa hakuna kinachoweza kuyafuta isipokuwa toba.

Kuonyesha Tafsiri

57 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
YO Yorùbá اليوروبا
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
SO Soomaali الصومالية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
CS Čeština التشيكية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
AZ Azərbaycan الأذربيجانية
UZ O‘zbek الأوزبكية
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
KMR Kurmancî الكرمنجية
Aina tofauti tofauti