Aina ndogo

Orodha ya Hadithi

1. Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kukimpendeza sana kuanzia kulia katika kuvaa kwake viatu, na kuchana kwake nywele, na kujisafisha kwake, na katika mambo yake yote. - 1 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
2. Mchungeni(mfuatilieni) Muhammadi -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa watu wa nyumba yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
3. Sikumuona Mtume -Rehema Amani ziwe juu yake- katu akipitiliza kucheka mpaka kionekane Kilimi ndani ya mdomo wake, bali alikuwa akitabasamu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
4. Msiziombee mabaya nafsi zenu,wala msiwaombee vibaya watoto wenu,wala msiziombee vibaya mali zenu,nakhofia dua hizo zisikutane na muda ambao haombwi Mwenyezi Mungu katika muda huo chochote isipokuwa anakujibuni.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
5. Atakapoona mmoja wenu ndoto anayoipenda, basi hiyo imetoka kwa Mwenyezi Mungu, na amshukuru Mwenyezi Mungu juu yake, na aisimulie
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
6. Atakayewalea mabinti wawili mpaka wakafikia utu uzima atakuja siku ya kiyama mimi na yeye ni kama vidole hivi viwili
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
7. Laiti nisingeliogopea uzito kwa umma wangu; ningeliwaamrisha kupiga mswaki kila wakati wa swala - 1 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
8. Hakuna siku ambayo wanaamka ndani yake waja isipokuwa kuna Malaika wawili wanateremka,anasema mmoja wao: Ewe Mwenyezi Mungu mpe mtoaji badala,na anasema mwingine:Ewe Mwenyezi Mungu mpe mzuiaji hasara
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
9. Nilikuwa kwa Saidi bin Jubair akasema: Ni nani kati yenu aliyeiona nyota iliyodondoka jana usiku? Nikasema: Mimi, kisha nikasema: Ama mimi sikuwa katika swala, lakini niling'atwa (na Nge)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
10. Fanyeni matendo na muwe na msimamo, na tambueni kuwa hatosalimika mmoja wenu kwasababu ya matendo yake, wakasema: Hata wewe Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?! Akasema: Hata mimi isipokuwa atakaponifunika mimi Mwenyezi Mungu kwa huruma zake na fadhila zake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
11. Allaahumma inni Audhubiridhwaaka min sakhatwika, -Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwa radhi zako kutokana na hasira zako, wabimuaafaatika min uquubatika,- Na kwa msamaha wako kutokana na adhabu zako-, Wa a'udhubika minka, -na ninajilinda kwako kwa ulinzi utokao kwako-, Laa uhswith thanaa 'alaika, -Siwezi kuzidhibiti shukurani zote juu yako, Anta kamaa athnaita a'laa nafsika, -Wewe kama ulivyojisifia nafsi yako
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
12. Hivi nisikuelezeni watu wa peponi? Kila mnyonge mwenye kujishusha, na lau kama angeliapia kwa Mwenyezi Mungu basi angelimuepusha na kila linalompa uzito, Hivi nisikuelezeni watu wa motoni? kila jeuri mkali mwenye kiburi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
13. Hakika mimi ninajua neno ambalo laiti angelisema yangemuondokea yaliyompata, lau angelisema: Au'dhubillaahi minshaitwanir-rajiim, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na shetani aliyelaaniwa, yangemuondokea yaliyompata
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
14. Ndoto nzuri hutoka kwa Mwenyezi Mungu, na njozi hutoka kwa shetani
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
15. Zuia ulimi wako, na ikutosheleze nyumba yako, na ulie juu ya makosa yako
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
16. Hakika peponi kuna daraja mia moja kaziandaa Mwenyezi Mungu kwaajili ya wenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu kati ya daraja mbili ni kama masafa ya baina ya mbingu na ardhi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
17. Amesema Mwenyezi Mungu -Mtukufu- mimi niko katika dhana ya mja wangu kwangu, na mimi niko pamoja naye pindi anaponikumbuka
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
18. Ni kwa jambo lipi alikuwa akianza nalo Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Anapoingia nyumbani kwake? Akasema: kwa mswaki
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
19. Huyo mtu kamkojolea shetani masikioni mwake, au alisema: sikioni kwake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
20. Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akifanya juhudi katika ramadhani kwa namna ambayo hajitahidi katika nyakati zingine nje ya ramadhani, na katika kumi la mwisho pia alikuwa na juhudi ambazo hakuwa anajitahidi hivyo nje ya ramadhani - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
21. Tulikuwa tukimuandalia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki wake na (maji yake kwaajili ya) twahara, basi Mwenyezi Mungu anamuamsha kwa muda anaotaka aamke nyakati za usiku, anapiga mswaki, na anatawadha na anaswali
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
22. Hato msitiri mja mja mwenzie duniani isipokuwa atamsitiri Mwenyezi Mungu siku ya kiyama
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
23. Asife mmoja wenu isipokuwa naye awe na dhana nzuri na Mwenyezi Mungu Mtukufu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
24. Ikiwa kama utakuwa kama ulivyosema, basi ni kana kwamba unawalisha majivu ya moto (dhambi wanazozipata ni kama mtu anayekula majivu ya moto), Na bado anaendelea kuwa pamoja nawe msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi yao, madam bado uko katika hali hiyo - 1 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
25. Haijawahi kupata vumbi miguu ya mja yeyote katika njia ya Mwenyezi Mungu, halafu ikaguswa na moto - 1 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
26. Hakuna watu wowote watasimama katika kikao ambacho hawamtaji Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani yake, isipokuwa watanyanyuka mithili ya mzoga wa punda, na wanakua na majuto
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
27. Mfano wa yule anayemtaja Mola wake na yule asiyemtaja Mola wake ni mfano wa aliyehai na aliyekufa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
28. Hakika katika yale ninayoyahofia zaidi kwenu nyinyi baada yangu ni yale yatakayofunguliwa kwenu miongoni mwa ua la dunia na pambo lake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
29. Atakayependa Mwenyezi Mungu amuokoe na Matatizo ya siku ya kiyama, basi amtatulie shida mwenye ugumu au ampunguzie
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
30. Hakika mwenye adhabu nyepesi zaidi katika watu wa motoni siku ya kiyama, ni mtu atawekewa ndani ya nyayo zake makaa mawili ya moto, utakuwa ukitokota kupitia hayo ubongo wake, na yeye atakuwa akiona kuwa hakuna mtu mwenye adhabu kali zaidi yake, na hakika kumbe yeye ndiye mwenye adhabu nyepesi kuliko wao
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
31. Atasogezwa muumini siku ya kiyama kwa Mola wake mpaka aweke upande wake kwake, kisha amtake akiri makosa yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa