1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti

Hadithi Utafuteni usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) katika witiri za kumi la mwisho katika Ramadhani

عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:

«تَحَرَّوْا لَيْلَةَ القَدْرِ فِي الوِتْرِ مِنَ العَشْرِ الأَوَاخِرِ مِنْ رَمَضَانَ».

Na imepokelewa kutoka kwa Aisha -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Utafuteni usiku wenye cheo (Lailatul Qadri) katika witiri za kumi la mwisho katika Ramadhani".

Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Swahiih Al Bukhaariy - 2017

Ufafanuzi

Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufanya juhudi kuutafuta usiku wenye cheo kwa kuzidisha amali njema, nao hutarajiwa zaidi kupatikana katika siku za witiri za siku kumi za mwisho wa Ramadhani kila mwaka, nazo ni: Ishirini na moja, na ishirini na tatu, na ishirini na tano, na ishirini na saba, na ishirini na tisa.

Katika Faida za Hadithi

  1. Fadhila za usiku wenye cheo (Lailatul-Qadri) na himizo la kuutafuta.
  2. Katika hekima za Mwenyezi Mungu na rehema zake aliuficha usiku huu ili watu wafanye jitihada katika ibada, kwa ajili ya kuutafuta, ili zikithiri thawabu zao.
  3. Usiku wenye cheo uko katika kumi la mwisho la Ramadhani, na katika siku za witiri ndio hutarajiwa zaidi.
  4. Usiku wenye cheo ni moja kati ya siku za kumi la mwisho la Ramadhani, nao ndio usiku ambao Mwenyezi Mungu aliiteremsha Qur'ani ndani yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akaufanya usiku huu kuwa ni bora kuliko miezi elfu moja katika baraka zake, na utukufu wa heshima yake, na athari ya matendo mema ndani yake.
  5. Umeitwa kuwa ni usiku wa Lailatul-Qadri, kwa kuiwekea sakna dali, ima ni kwa sababu ya utukufu wake, husemwa: Fulani anacheo kikubwa, inakuwa kuuambatanisha usiku ni katika sehemu ya kuambatanisha kitu katika sifa yake, yaani usiku mtukufu, yaani unacheo kikubwa kwa utukufu na thamani na nafasi mpaka mwisho wake, "Hakika sisi tumeiteremsha katika usiku wenye baraka" [Ad-Dukhan: 3]. Na ima imetokana na kukadiria: Inakuwa kuambatanishwa kwake ni kuambatanishwa kwa kuambatana na kile kinachokizunguka, yaani ni usiku ambao ndani yake kunakuwa na makadirio ya yale yatakayoendelea katika mwaka mzima, "Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hekima" [Ad-Dukhan: 4].

Kuonyesha Tafsiri

47 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
NE नेपाली النيبالية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
Aina tofauti tofauti