Aina:
عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، قَالَتْ:

مَا رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُسْتَجْمِعًا قَطُّ ضَاحِكًا، حَتَّى أَرَى مِنْهُ لَهَوَاتِهِ، إِنَّمَا كَانَ يَتَبَسَّمُ.
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Sikumuona Mtume -Rehema Amani ziwe juu yake- katu akipitiliza kucheka mpaka kionekane Kilimi ndani ya mdomo wake, bali alikuwa akitabasamu.
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Hadithi ya Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- inatupa picha ya baadhi ya pande za muongozo wa utume katika tabia za unyenyekevu na utulivu akasema -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: "Sikumuona Mtume -Rehema Amani ziwe juu yake- katu akipitiliza kucheka mpaka kionekane Kilimi ndani ya mdomo wake, bali alikuwa akitabasamu" Anakusudia hacheki kicheko cha uovu kilichoambatana na kukuhoa, afungue mdomo wake mpaka ionekane sehemu ya ndani ya sakafu ya mdomo, lakini yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa akitabasamu au akicheka mpaka yanadhihiri magego yake, au yanaonekana meno yake ya mbele, na hii ni katika unyenyekevu wa Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake-.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama

Maana ya Maneno

Aina tofauti
Ziada