«تَفْضُلُ صَلاَةُ الجَمِيعِ صَلاَةَ أَحَدِكُمْ وَحْدَهُ، بِخَمْسٍ وَعِشْرِينَ جُزْءًا، وَتَجْتَمِعُ مَلاَئِكَةُ اللَّيْلِ وَمَلاَئِكَةُ النَّهَارِ فِي صَلاَةِ الفَجْرِ» ثُمَّ يَقُولُ أَبُو هُرَيْرَةَ: فَاقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: {إِنَّ قُرْآنَ الفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا} [الإسراء: 78].
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 648]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Imekuwa ni bora swala ya wengi kuliko swala ya mmoja wenu peke yake, kwa vipengele ishirini na tano, na hukusanyika Malaika wa usiku na Malaika wa mchana katika swala ya Alfajiri" Kisha anasema Abuu Huraira: Someni mkitaka: "Hakika Qur'ani ya Alfajiri hushuhudiwa" [Al-Israa: 78].
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 648]
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba thawabu na malipo ya swala ya mtu katika jamaa pamoja na imamu ni bora kuliko swala ishirini na tano anazoziswali peke yake nyumbani kwake au sokoni kwake, kisha akataja rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika wa usiku na mchana hukusanyika katika swala ya Alfajiri, kisha anasema Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake akitoa ushahidi kwa hilo:
Someni mkitaka: "Hakika Qur'ani ya Alfajiri hushuhudiwa" [Al-Israa: 78] Yaani: Qur'ani ya Alfajiri huishuhudia Malaika wa usiku na Malaika wa mchana.