1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti

Hadithi Neema mbili wamepoteza thamani yake watu wengi: Afya na wakati

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:

«نِعْمَتَانِ مَغْبُونٌ فِيهِمَا كَثِيرٌ مِنَ النَّاسِ: الصِّحَّةُ وَالفَرَاغُ».

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Neema mbili wamepoteza thamani yake watu wengi: Afya na wakati".

Sahihi Imepokelewa na Al-Bukhaariy Swahiih Al Bukhaariy - 6412

Ufafanuzi

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu neema mbili kubwa miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu kuwa wanapata hasara ndani yake watu wengi, kiasi kwamba wanazitumia mahali pasipostahiki; kwani mwanadamu zikikusanyika kwake neema ya afya na wakati, akazidiwa na uvivu wa kufanya ibada basi kapata hasara; na ndio hali ya watu wengi, na akiutumia muda wake na afya yake katika kumtii Mwenyezi Mungu basi atakuwa kapata faida; hii ni kwa sababu dunia ndio shamba la Akhera, na wakati hufuatiwa na shughuli, na afya hufuatiwa na maradhi, na lau kusingekuwa na chochote zaidi ya uzee basi ungetosha.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumfananisha mtu mzima na mfanya biashara, na afya na muda kavifananisha na mtaji; atakayeutumia vizuri mtaji wake atapata faida, na atakayeupoteza basi atapata hasara na kujuta.
  2. Amesema bin Khaazin: Neema ni kila anachoneemeka nacho mtu na anapata ladha kwacho, na udanganyifu, ni mtu kununua kitu kwa thamani kubwa, au kukiuza kwa thamani isiyolingana na kilichouzwa; atakayekuwa na afya katika mwili wake na akawa na wakati na hana la kumshughulisha, na akawa hakwenda mbio kuitumikia Akhera yake huyu ni sawa na aliyefanya biashara yenye udanganyifu.
  3. Kuwa na pupa ya kufaidika na afya na wakati kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka, na kufanya kheri kabla ya kutoweka kwake.
  4. Kushukuru neema za Mwenyezi Mungu kunakuwa kwa kuzitumia katika kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  5. Amesema Kadhi Abubakari bin Al-Arabi: Kumepatikana tofauti kuwa ni ipi neema ya kwanza kwa mja, kukasemwa: Ni imani, na kukasemwa: Ni uhai, na kukasemwa: Ni afya, na ya kwanza ndio bora kwa sababu ndio neema ya kiujumla, na ama uhai na afya hizo ni neema za kidunia, na wala haziwezi kuwa neema halisia isipokuwa zitakapoambatana na imani, na hapo ndipo wanapohadaika watu wetu, yaani inapotea faida yao au inapungua, atakayeiendekeza nafsi yake yenye kuamrisha maovu, na yenye kudumu katika starehe, akaacha kuhifadhi mipaka ya Mwenyezi Mungu, na kudumu na ibada, basi huyu atakuwa kahadaika, na vile vile atakapokuwa hana la kumshughulisha, kwa sababu aliyeshughulishwa anaweza kuwa na udhuru tofauti na mwenye nafasi; basi huyu hana udhuru na hoja itasimama juu yake.

Kuonyesha Tafsiri

47 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
NE नेपाली النيبالية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
Aina tofauti tofauti