1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti

Hadithi Allah amng'arishe mtu aliyesikia kutoka kwangu chochote akakifikisha kama alivyo sikia, huenda mfikishiwa akawa mwerevu zaidi kuliko aliye sikia

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:

«نَضَّرَ اللَّهُ امْرَأً سَمِعَ مِنَّا شَيْئًا فَبَلَّغَهُ كَمَا سَمِعَ، فَرُبَّ مُبَلِّغٍ أَوْعَى مِنْ سَامِعٍ».

Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Allah amng'arishe mtu aliyesikia kutoka kwangu chochote akakifikisha kama alivyo sikia, huenda mfikishiwa akawa mwerevu zaidi kuliko aliye sikia".

Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad Sunanu Tirmidhiy - 2657

Ufafanuzi

Aliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kung'arisha na muonekano na uzuri katika dunia, na amfikishe Mwenyezi Mungu katika mng'ao wa peponi na neema zake na mng'ao wake katika Akhera; kwa yule atakayesikia hadithi yake akaihifadhi ili amfikishie mwingine, huenda aliyenukuliwa hadithi akawa mwerevu na muelewa na akawa na uwezo wa kuchambua hukumu kuliko hata aliyeinukuu hadithi, akawa wa kwanza anahifadhi vizuri, na wa pili akawa anauelewa na uchambuzi mzuri.

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kuhifadhi mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kuyafikisha kwa watu.
  2. Kumebainishwa fadhila za watu wa hadithi, na heshima ya kuitafuta kwake.
  3. Fadhila ya wanachuoni, ambao wanastahiki kuchambua na kuzielewa hadithi.
  4. Ubora wa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, wao ndio waliosikia hadithi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wakatufikishia.
  5. Amesema Al-Munaawi: Amebainisha kuwa mpokezi wa hadithi kuwa na uelewa si katika sharti zake, bali sharti lake ni kuhifadhi, na kwa msomi kuelewa na kuzingatia.
  6. Amesema bin Uyaina: Hakuna yeyote anayetafuta hadithi isipokuwa kuna mng'ao katika uso wake kwa hadithi hii.
  7. Kuhifadhi kwa wasomi wa hadithi kuna aina mbili: Kuhifadhi kwa moyo na kifua, na kuhifadhi kwa kitabu na mwandiko, na aina zote mbili zinakusanywa na dua iliyoko katika hadithi.
  8. Ufahamu wa watu unatofautiana, huenda mfikishiwa akawa muelewa zaidi kuliko aliyesikia, na huenda aliyebeba maarifa ya sheria akawa si muelewa.

Kuonyesha Tafsiri

46 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
NE नेपाली النيبالية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
Aina tofauti tofauti