Aina:
+ -
عَن عَبْدِ اللهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رضي الله عنهما أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُ:

«إِنَّ قُلُوبَ بَنِي آدَمَ كُلَّهَا بَيْنَ إِصْبَعَيْنِ مِنْ أَصَابِعِ الرَّحْمَنِ، كَقَلْبٍ وَاحِدٍ، يُصَرِّفُهُ حَيْثُ يَشَاءُ» ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «اللهُمَّ مُصَرِّفَ الْقُلُوبِ صَرِّفْ قُلُوبَنَا عَلَى طَاعَتِكَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2654]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Amri bin Aaswi -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake akisema:
"Hakika nyoyo za wanadamu zote ziko baina ya vidole viwili miongoni mwa vidole vya Rahmaan (Mwingi wa rehema), kama moyo wa mtu mmoja, anaugeuza kokote atakako" Kisha akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu mwenye kuzigeuza nyoyo, zigeuze nyoyo zetu zielekee katika kukutii".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2654]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa nyoyo za wanadamu zote ziko baina ya vidole viwili katika vidole vya Rahmaan kama moyo mmoja; anaugeuza kokote atakako; akitaka anausimamisha katika haki, na akitaka anaupotoa katika haki, na kuzigeuza kwake nyoyo zote ni kama kuugeuza moyo mmoja, hakuna jambo linaloweza kumshughulisha akaacha jambo jingine, kisha akaomba rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ewe Mwenyezi Mungu mwenye kuzigeuza nyoyo, wakati mwingine katika utiifu na wakati mwingine katika maasi, na wakati mwingine katika kukutaja na wakati mwingine katika kughafilika, zigeuze nyoyo zetu zielekee katika utiifu wako.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumethibitishwa makadirio, nakuwa Mwenyezi Mungu anazielekeza nyoyo za waja wake kulingana na kadari aliyoziandikia juu yake.
  2. Inampasa muislamu kudumu kumuomba Mola wake Mlezi kuthubutu katika haki na uongofu.
  3. Kumhofu Mwenyezi Mungu na kufungamana nayeye peke yake asiye na mshirika.
  4. Amesema Aajurri: Hakika watu wa haki humsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa sifa alizojisifu mwenyewe Aliyetakasika na kutukuka, na kwa sifa alizomsifu kwazo Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, na kwa zile walizomsifu kwazo Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na huu ndio msimamo wa wanachuoni katika wale waliofuata muongozo na wala hawakuzua. Mwisho. Watu wa sunna humthibitishia Mwenyezi Mungu aliyoyathibitisha yeye mwenyewe kwa nafsi yake katika majina na sifa pasina kupotoa, wala kukanusha wala kuhoji wala kufananisha, na wanamkanushia Mwenyezi Mungu yale aliyoyakanusha yeye mwenyewe juu nafsi yake, na wananyamaza katika yale ambayo mafundisho hayakueleza kuthibitisha au kukanusha, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakuna chochote mfano wake, naye ni Msikivu Mwenye kuona".
الملاحظة
قال الآجري: إن أهل الحق يَصِفُوْن الله عز وجل بما وصف به نفسه عز وجل، وبما وصفه به رسوله صلى الله عليه وسلم، وبما وصفه به الصحابة رضي الله عنهم، وهذا مذهب العلماء ممن اتبع ولم يَبتدِع. انتهى. فأهل السنة يُثْبِتُوْن لله ما أثبته لنفسه من الأسماء والصفات من غير تحريف ولا تعطيل ولا تكييف ولا تمثيل، ويَنْفُون عن الله ما نفاه عن نفسه، ويَسكتون عما لم يَرِدْ به نفيٌ ولا إثبات، قال الله تعالى: (‌لَيْسَ ‌كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ).
لا حاجة لأبينها إذ لم يتجرأ أحد من السلف بأن قال أصبعان حقيقيان وإنما قالوا أصبعان لا نعلمهما. هذا وإن المنصفين يعلمون أن الخلف وإن أوّلوا المعنى بالقدرة والإرادة فهم: لم ينكروا أن له أصبعين لكن رفضوا أن يكون المعنى على ظاهره لقرينة منعت ذلك. لم يأتوا بمعنى مخالف لظاهر الحديث فهو يفيد قدرة الله وإرادته في عباده وهذا ما تأولوا معناه هذا وإن المخالفين لهم حتى وإن أثبتوا الأصبعين الحقيقيين الذين نعلمهما فإنهم لا مفرّ لهم من تأول المعنى
النص المقترح لا يوجد...
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kiassam الهولندية الغوجاراتية الرومانية المجرية الموري الجورجية
Kuonyesha Tarjama
Aina tofauti
Ziada