1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti

Hadithi Nilishuhudia swala ya Idd pamoja na Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Siku mbili hizi alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufunga ndani yake: Siku ya kufungua kwenu kutoka katika swaumu yenu, na siku nyingine ni ile mnayokula katika vichinjwa vyenu

عَنْ أَبِي عُبَيْدٍ، مَوْلَى ابْنِ أَزْهَرَ، قَالَ:

شَهِدْتُ العِيدَ مَعَ عُمَرَ بْنِ الخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، فَقَالَ: هَذَانِ يَوْمَانِ نَهَى رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ صِيَامِهِمَا: يَوْمُ فِطْرِكُمْ مِنْ صِيَامِكُمْ، وَاليَوْمُ الآخَرُ تَأْكُلُونَ فِيهِ مِنْ نُسُكِكُمْ.

Kutoka kwa Abuu Ubaidi, mwachwa huru wa bin Azhari, amesema:
Nilishuhudia swala ya Idd pamoja na Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Siku mbili hizi alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufunga ndani yake: Siku ya kufungua kwenu kutoka katika swaumu yenu, na siku nyingine ni ile mnayokula katika vichinjwa vyenu.

Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Swahiih Al Bukhaariy - 1990

Ufafanuzi

Alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufunga siku ya Iddil-Fitiri na Iddil-Adh-ha; ama Iddil-Fitiri ni siku ya kufungua kutoka katika swaumu ya mwezi wa Ramadhani, na ama Iddil-Adh-ha ni siku ya kula katika vichinjwa.

Katika Faida za Hadithi

  1. Uharamu wa kufunga siku mbili za Iddil-Fitiri na Iddil-Adh-ha, na siku tatu za kubanika nyama; kwa sababu zinafuatana na siku ya Iddil-Adh-ha isipokuwa kwa yule ambaye hakupata cha kutoa, itafaa kwake kufunga siku za kubanika nyama.
  2. Amesema bin Hajari: Imesemekana kuwa: Na faida ya kuzitaja siku mbili ni ishara ya kuonyesha sababu ya uwajibu wa kufungua ndani yake, nazo ndio mapumziko ya swaumu, na kudhihirisha ukamilifu wake peke yake kwa kufungua siku zilizo baada yake, na Idd nyingine ni kwa ajili ya kuchinja kwa mwenye kujikurubisha kwa kichinjwa chake ili ale kutoka katika kichinjwa hicho.
  3. Inapendeza kwa mtoa hotuba ataje katika hotuba yake yale yanayohusiana na wakati wake miongoni mwa hukumu, na atumie fursa ya matukio kama hayo.
  4. Sheria ya kula kutoka katika kichinjwa cha ibada.

Kuonyesha Tafsiri

47 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
NE नेपाली النيبالية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
Aina tofauti tofauti