Aina ndogo

Orodha ya Hadithi

1. Ibada ya Umra ndani ya ramadhani inalingana na Hija -au Hija pamoja nami.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
2. Alikuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akikaa itikafu katika kila ramadhani siku kumi, ulipofikia mwaka aliofishwa ndani yake alikaa itikafu siku ishirini
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
3. Kwenu nyinyi jihadi bora: ni hija njema
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
4. Atakayepigana ili liwe neno la Mwenyezi Mungu ndio la juu basi huyo yuko katika njia ya Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
5. Msivae hariri nyepesi wala nguo zilizofumwa kwa hariri, na wala msinywe katika vyombo vya dhahabu wala fedha, na wala msile katika sahani zake, kwani hivyo ni vyao duniani na ni vyenu Akhera
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
6. Atakaye apa juu ya kiapo cha mila isiyokuwa ya uislamu kwa uongo tena kwa makusudi basi atakuwa kama alivyosema - 2 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
7. Alitoka Muawiya- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akakuta duara msikitini, akasema: Nini kimewakalisheni? wakasema: tumekaa tunamtaja Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
8. Nyoosheni safu zenu, kwani hakika kunyoosha safu ni katika ukamilifu wa swala - 1 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
9. "Haya (Aibu) haiji ila kwa kheri" - 1 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
10. Hachukii muumini wa kiume tabia za muumini wa kike, akichukia tabia fulani basi ataridhishwa na tabia nyingine. Au alisema:tofauti na hiyo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
11. Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akaenda haja ndogo, akatawadha, na akafuta juu ya khufu zake (viatu vya ngozi mfano wa soksi).
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
12. Mtakapokwenda haja kubwa, msielekee kibla kwa haja kubwa wala ndogo, na wala msikipe kibla mgongo, lakini elekeeni mashariki au magharibi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
13. Asishike mmoja wenu utupu wake kwa mkono wake wa kulia akiwa anakidhi haja ndogo, na asijifute haja ndogo au kubwa kwa mkono wake wa kulia na asipumulie ndani ya chombo anachonywea.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
14. Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Alikuwa akinyanyua mikono yake usawa wa mabega yake anapofungua swala, na anapotoa takbira ya kurukuu, na anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu anainyanyua pia
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
15. Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimuweka fidia baba yangu na mama yangu, Hebu nieleze kunyamaza kwako kati ya takbira na kisomo: Ni nini unasema: Akasema: Ninasema: Allaahumma baaid bainiy -Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali baina yangu- wa baina khatwaayaaya -na baina ya makosa yangu- kamaa baa a'tta bainal mashriqi wal maghribi -kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Allaahumma naqqiniy- Ewe Mwenyezi Mungu nitakase mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- kamaa yunaqqaath-thaubul abyadhwa -kama inavyotakaswa nguo nyeupe- minad danasi -kutokana na uchafu. Allaahumma ghsilniy -Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- bil maai wath thalji wal baradi -kwa maji na barafu na baridi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
16. Hivi nikuhadithieni hadithi kuhusu Dajali ambayo hajawahi kuhadithia Nabii yeyote watu wake! Hakika yeye ni chongo, na hakika yeye atakuja akiwa pamoja na mfano wa pepo na moto, anayoisema kuwa ni pepo huo ndio moto
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
17. Linganeni sawa katika sijida, na asikunjue mmoja wenu mikono yake kama anavyokunjua mbwa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
18. Hakika bila shaka mfano wa rafiki mwema na rafiki muovu, ni kama mfano wa mbeba miski, na mfua vyuma - 1 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
19. Fanyeni haraka kufanya matendo kuna fitina nzito kama kipande cha usiku wa giza, anaamka mtu akiwa muislamu anafika jioni akiwa kafiri, na anashinda akiwa muumini anaamka asubuhi akiwa kafiri, anauza dini yake kwa thamani ndogo ya dunia - 1 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
20. Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa anapo swali anatanua kati ya mikono yake mpaka unaonekana weupe wa kwapa lake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
21. Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na Dinari anayoitoa kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na Dinari anayoitoa kwa jamaa zake katika njia ya Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
22. Ajabu iliyoje ya jambo la muumini, hakika jambo lake lote ni kheri, na hakuna hilo kwa yeyote ila kwa muumini: akipatwa na jambo lenye kufurahisha anashukuru ikawa hilo ni kheri kwake, na akipatwa na madhara anasubiri likawa hilo ni kheri kwake. - 1 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
23. Kiliwekwa kwaajili ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- chombo cha kuogea janaba, akamimina kwa mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto mara mbili -au tatu- kisha akaosha tupu yake, kisha akapiga ardhi kwa mkono wake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
24. Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au nguo yake juu ya kinywa chake, na anapunguza sauti yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
25. Hakika mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu, kiwango cha unyoya wa mshale (Yaani: taratibu taratibu), hata watakapoingia katika shimo la kenge mtaingia. Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, (Unakusudia) Mayahudi na Manaswara? Akasema: Akina nani wengine (kama si hao!)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
26. Nyanyua kichwa chako na sema yasikilizwe, na omba upewe, na taka utetezi utetewe
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
27. Hakuna kuambukizana maradhi wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, wala mkosi wa Bundi,na aina zingine za ndege,wala kutuhumu kuwa mwezi wa safari unamikosi, au maradhi ya tumbo yanayompata ngamia.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
28. Nitampa bendera kesho mtu ambaye anampenda Allah na Mtume wake,na anapendwa na Allah na Mtume wake,kupitia yeye Allah ataleta ushindi. - 1 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
29. Hakika watu watakapomuona mtu dhalimu (muovu) na wakawa hawakumzuia wako karibu mno, Mwenyezi Mungu kuwafunika wote kwa adhabu itokayo kwake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
30. Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mtaamrisha mema, na mtakataza mabaya; au hakika atakuwa karibu zaidi Mwenyezi Mungu kukutumieni adhabu toka kwake, kisha mtamuomba na wala hamtojibiwa - 1 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
31. Je! nikujulisheni mambo ambayo yakifanyika Allah hufuta madhambi na hupandisha daraja kwa mambo hayo? wakasema: ndiyo, Ewe Mtume wa Allah, akasema: Kutawadha vizuri wakati wa baridi, na kuzidisha hatua kwenda msikitini, na kusubiria swala baada ya swala huko ndiko kuizuia nafsi katika mambo ya kheri.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
32. Je nikujulisheni matendo yenu bora, na matukufu mbele ya mfalme wenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
33. Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kutoka maeneo ya Najid, kichwa chake kikiwa kimetimka, tunasikia mvumo wa sauti yake, na wala hatuelewi anasema nini, mpaka akasogea karibu kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ghafla akaanza kuuliza kuhusu uislamu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
34. Siku bora lililochomoza jua ndani yake ni siku ya ijumaa: Ndani yake kaumbwa Adam, na ndani yake kaingizwa peponi, na ndani yake katolewa humo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
35. Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), kisha Ameangukia pua (kapata hasara), atakayewapata wazazi wake wawili wakati wa ukubwa mmoja wao au wote wawili na akawa hakuingia peponi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
36. Wametangulia watu wa kipekee
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
37. Shikamana na kukithirisha kusujudu; kwani wewe hutosujudu kwaajili ya Mwenyezi Mungu sijida moja isipokuwa atakunyanyua Mwenyezi Mungu kwa hiyo sijida daraja moja, na anakufutia kwa hiyo dhambi moja
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
38. Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani mwenye haki zaidi ya kumfanyia wema wa karibu? akasema: mama yako, kisha mama yako kisha mama yako, kisha baba yako, kisha anayefuata kwa ukaribu kisha nayemfuata kwa ukaribu - 3 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
39. Atakayeswali (katika nyakati mbili) za baridi ataingia peponi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
40. Muislamu atakapoulizwa kaburini anashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hiyo ndiyo kauli yake Mtukufu: "Huwapa umakinifu Mwenyezi Mungu wale walioamani kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika akhera
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
41. Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa - 1 ملاحظة
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa