عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:

«لَتَتَّبِعُنَّ سَنَنَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ، شِبْرًا بِشِبْرٍ، وَذِرَاعًا بِذِرَاعٍ، حَتَّى لَوْ دَخَلُوا فِي جُحْرِ ضَبٍّ لَاتَّبَعْتُمُوهُمْ» قُلْنَا: يَا رَسُولَ اللهِ آلْيَهُودَ وَالنَّصَارَى؟ قَالَ: «فَمَنْ؟».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abii Saidi Al khudriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Hakika mtafuata nyenendo za wale waliokuwa kabla yenu, kiwango cha unyoya wa mshale (Yaani: taratibu taratibu), hata watakapoingia katika shimo la kenge mtaingia". Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, (Unakusudia) Mayahudi na Manaswara? Akasema: "Akina nani wengine (kama si hao!)".
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim kwa riwaya zake

Ufafanuzi

Anatueleza Abuu Saidi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- alieleza kuwa umma huu utakuja kuiga umma zilizotangulia katika desturi zake na siasa zake na dini zake, na kuwa wao watajaribu kuwaiga katika kila kitu, kama unyoya wa mshale unavyofanana na manyoya mengine, kisha akasisitiza mfanano na kuiga huku kuwa umma zilizopita lau ataingia shimo la kenge pamoja na udogo wake na giza lake ungejaribu umma huu pia kuingia, na walipotaka ufafanuzi maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuhusu makusudio ya wale waliokuwa kabla yao, na je ndio mayahudi na wakristo? Akajibu kwa ndiyo.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Thai Kiassam الدرية
Kuonyesha Tarjama

Maana ya Maneno

قال فمن؟:
استفهامٌ إنكاريٌّ أي: فمن هم غيرُ أولئك.